NAIBU WAZIRI UMMY MWALIMU AWATAKA WADAU KUUNGANISHA NGUVU ILI KUFANIKISHA KAMPENI YA BIAAG.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Duniani iliyokwenda sambamba na Uzinduzi wa Kampeni ya ‘Because I am a Girl’ (BIAAG) ambapo amesema upo umuhimu wa kuandaa mijadala kitaifa kuhusu masuala ya haki za watoto kwa kuwakutanisha pamoja watoto wote, wakime wadau, wizara mbali mbali. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Plan International Tanzania Bw. David Muthungu.
Kauli Mbiu ya Mwaka Huu ni “ Maisha Yangu, Haki Yangu, Tokomeza Ndoa za Utotoni”
Mkurugenzi wa Shirika la Plan International Tanzania Bw. David Muthungu akitoa hotuba wakati wa maadhimisho hayo ambapo amesema Siku Hii ilipitishwa rasmi na Umoja wa Mataifa na kuwa ni siku maalum sana ambayo inatoa fursa kwa wadau wote wa haki za watoto na haki za binadamu duniani kote kupaza sauti dhidi ya changamoto zinazo wakabili watoto wa kike.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Mh. Ummy Mwalimu (kulia) na Mkurugenzi wa Shirika la Plan International Tanzania Bw. David Muthungu wakizindua rasmi kampeni ya‘Because I am a Girl’ (Kwa sababu Mimi Ni Msichana) BIAAG ambayo ni kampeni ya ya dunia ya Shirika la Kimataifa la Plan inayoanza Oktoba 2012 ha di Juni 2016. Kampeni hii inalenga kupambana na unyanyasaji wa kijinsia, kukuza haki za wasichana na kuinua mamilioni ya wasichana kutoka katika umasikini.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya Wadau wa haki za Watoto waliohudhuria uzinduzi huo.
Mh. Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na Bw. David Muthungu na wanafunzi pamoja na wadau wa kampeni hiyo baada ya uzinduzi rasmi.
No comments:
Post a Comment