MKUTANO WA “CAUCUS” WAKAMILIKA.
Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa akiwa pamoja na Gavana wa Benki kuu Bw. Benno Ndulu kwenye mkutano wa Mawaziri wa Afrika wakifuatilia mkutano wa Mawaziri wa Afrika ( Caucus meeting) ambapo majadiliano hayohuafikiwa kwa pamoja na kupelekwa ngazi za juu za uongozi wa IMF.Mkutano huo ulifanyika leo jijini Tokyo-Japan.
Mawaziri wa Fedha wa Afrika katika mkutano wa pamoja wa Mawaziri Jijini Tokyo- Japan,mkutano huo unajulikana kama (Caucus meeting).
Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa na Profesa Benno ndulu katika mkutano wa pamoja wa mawaziri wa Afrika, Jijini Tokyo- Japan.
Viongozi wa Afrika wanaoongoza mkutano wa Mawaziri wa Afrika, Jijini Tokyo- Japan.(Picha na Ingiahedi Mduma na Scola Malinga).
Mikutano ya IMF inaendelea, wakati huo huo mikutano mingine ikichukua nafasi yake na kusaidia kujadili mambo ambayo yanaweza yakalisaidia Bara la Afrika.
Mawaziri wa Fedha wa Afrika wakiambatana na Magavana wao wa Benki kuu leo wamehudhuria mkutano wa “CAUCUS”.
Mikutano hii inafanyika kwa lengo la kuwakutanisha Mawaziri wote wa Afrika ili kuweza kuzungumzia matatizo yao kwa ujumla na wakisha yakamilisha huyachambua na kuyapeleka kama ripoti moja kwa Rais wa Benki ya Dunia na kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimatafa.Katika kikao hicho, Mawaziri hao wanazungumzia ni jinsi ni gani Taasisi hizo mbili zinavyoweza kuzitoa Nchi za Afrika na ni maeneo gani ambayo Afrika ikisaidiwa inaweza kuendelea.
No comments:
Post a Comment