KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Saturday, 13 October 2012


Tanzia: Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza auawa

 
Picture
Liberatus Barlow
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Barlow ameuawa saa tisa usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa blogu ya Said Powa na tovuti ya gazeti la Habari Leo:

 Tukio hilo linahusishwa na ujambazi.

Taarifa kutoka Mwanza ambazo zimethibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema, zinasema kuwa Kamanda Barlow wakati akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake akitoka kumrudisha dada yake ambaye alikuwa kwenye kikao cha harusi ya ndugu yao huko Kitangili.

Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai DCI Robert Manumba akiwa na kikosi cha makachero tayari wameshakwenda mwanza kuongeza nguvu katika upelelezi mkali ambao umekwishaanza.

---

Kwa mujibu wa blogu ya CCM Chama:

Kamanda Barlow alipigwa risasi na watu wasiojulikana kiasi cha saa sita usiku, atika eneo la Kitangiri, kwenye kona ya Bwiru, Mwanza.

Inadaiwa kuwa Kamanda huyo alikuwa akimwendesha mwanamke mmoja ambaye bado hajatambulika, akimpeleka nyumbani kwake baada ya kutoka kwenye sherehe ya harusi.

“Inadaiwa kwenye harusi hiyo kuna mwanamke alimwomba ampeleke nyumbani, akamchukua katika gari na kumpeleka, walipofika eneo la Kitangiri, pale kona ya Bwiru, walitokea watu ambao wamempiga risasi moja shingoni...” (amesema mtoa habari kutoka Mwanza).


No comments:

Post a Comment