BUNGE LA TANZANIA MFANO WA KUIGWA KATIKA KUWASHIRIKISHA WANAWAKE.
Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) akiongozana na Balozi wa Tanzania nchini India, Engineer John Kijazi, wakati wakuingi a katika ukumbi wa utamaduni wa Kihindi katika viwanja vya Bunge la India mjini New Delhi.
Wakiwa kwenye vazi maalumu waliloandaliwa, kutoka kulia ni Spika wa Bunge la India na mwenyeji wa mkutano wa Saba wa Maspika wanawake duniani Mhe. Meira Kumar, Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda na spika wa Bunge la Swaziland Mhe Gelane T. Zwane.
Rais wa Inter-Parliamentary Union (IPU), Bw. Abdelwahad Radi (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu wa IPU Bw. Anders Johnsson ni miongoni mwa viongozi mashuhuri waliohudhuria mkutano huo unaosisitiza wanawake kupewa nafasi zaidi katika vyombo vya maamuzi.
Mapema akihutubia mkutano huo Spika Makinda aliwaambia wajumbe kuwa wabunge wanawake Tanzania ni 36% jambo ambalo lilifanya Tanzania kusifiwa na kushauriwa kusonga mbele hadi 50%.
Picha ya pamoja ya baadhi ya maspika wanawake wa IPU ndani ya vazi maalumu waliloandaliwa.(Prosper Minja).
No comments:
Post a Comment