Pichani Juu na Chini ni Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, John Samwel Malecela akimtunuku Shahada ya Uongozi wa  Biashara, Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda katika Mahafali ya Chuo Kikuu Huria  yaliyofanyika kwenye viwanja vya Chuo hicho Kibaha Oktoba 27, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akipokea  zawadi ya ua kutoka wadogo zake Salma Rehani (kulia), Mkaroga Rehani (wapili kulia) na Mabe Rehani baada ya kutunukiwa Shahada ya Uongozi wa Biashara  katika mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye vianja vya Chuo hicho, Kibaha.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza, Papius Yachitwi  ambaye alitunukiwa BA in Linguistic katiak Mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyofanyika kwenye  vianja vya Chuo hicho, Kibaha Octoba 27, 2012. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho, John Samwel Malecela.
Baadhi ya Wahitimu wa Chuo Kikuu Huria Cha Tanzania Wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ((hayupo pichani) wakati alipowahutubia kwenye mahafali ya Chuo hicho yaliyofanyika Kibaha.
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal akimpongeza kwa zawadi Mama Tunu Pinda.