Dkt. Ulimboka Stephen
12/08/2012
Daktari Ulimboka hapa akiwasihi ndugu zake pamoja na Madaktari wamwache azunguimze kidogo na waandishi ili akate kiu yao baada ya kusubiri uwanjani hapo kwa muda mrefu, lakini ndugu na madaktari hao wakionekana kipinganaye na kumtaka aende akapumzike na taarifa zote zitolewe baadaye, hata hivyo alizungumza na waandishi baada ya mvutano wa muda kidogo. (picha: Raha za Pwani blog)
Na, Waandishi wa GlobalPublishers.info,
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini Tanzania, Dkt. Ulimboka Stephen, amerejea salama nchini leo mchana na kutoa shukrani za dhati kwa Watanzania kwa dua na michango yao kuinusuru afya yake na kuahidi kuendeleza mapambano dhidi ya huduma bora za afya na maslahi kwa Madaktari.
Dkt. Ulimboka, aliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, saa 8:00 mchana na ndege ya Shirika la SA Airways, akitokea nchini Afrika Kusini, alipokwenda kwa matibabu.
Madaktari wenzake, ndugu, jamaa, marafiki, Wanaharakati na wananchi wengine, walimlaki kwa shangwe, hoihoi, nderemo huku wakiwa na mabango yenye ujumbe ambao GlobalPublishers.info imenukuu kuwa ulisomeka:
“DR. Ulimboka karibu nyumbani.”
“DR. Ulimboka, damu yako iliyomwagika inaamsha ari ya wananchi kudai haki ya afya.”
“DR. Ulimboka wewe ni mpigania haki ya afya bora kwa wananchi wote. Mungu na Watanzania wote tuko nawe.”
Kwa upande mwingine, Dkt. Ulimboka baada ya kukuta umati mkubwa uwanjani, alishindwa kujizuia, hivyo akatoa machozi kisha akasema: “Nawashukuru sana Watanzania kwa kuwa pamoja na mimi kwa maombi, sasa nimerejea nikiwa na afya njema, mapambano yanaendelea,” na kuongeza: “Watu wacheze na watu lakini wasicheze na Mungu, hasa Mungu wangu mimi.”

Dkt. Ulimboka ambaye amejizolea umaarufu nchini kwa harakati za kudai haki na maslahi ya Madkatari na huduma bora Hospitalini, amerejea nchini wakati jamii bado ikiwa katika kizungumkuti cha nani hasa aliyemteka na kumpa mateso makali huku kiu ya wananchi sasa ikiwa ni kutaka kujua ukweli kupitia kwake.
Licha ya vurugu za hapa na pale ambazo zilikuwa zikisababishwa na ndugu na jamaa ambao walitaka wanahabari wasilidake tukio hilo la kihistoria paparazi waliweza kunasa taswira kadhaa na kuongea naye, “Nimepona ndugu zangu… nawashukuru nyote mlioniombea, Watanzania, Madaktari, ndugu na jamaa zangu nashukuru pia kunisaidia kupata matibabu bora hadi leo hii narudi nyumbani, niko fiti nikitembea mwenyewe,” alisema Dkt. Ulimboka.
Miongoni mwa wanaharakati ambao "Father Kidevu Blog" ilifanikiwa kuwaona uwanjani hapo ni pamoja na Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Usu Mallya na Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake (TAMWA), Ananileya Nkya.
Wanaharakati hao walijipamba na mabango kadhaa yaliyo kuwa na jumbe za “Dkt. Ulimboka karibu nyumbani uliumizwa kikatili ukitetea afya bora kwa watanzania.” “Dkt. Ulimboka damu yako ilimwagika na kuamsha ari kwa wananchi kudai huduma bora za afya.” “Dkt. Ulimboka wewe ni mpigania haki na afya bora kwa wananchi wote Mungu na watanzania wote tuko nawe.”
Naye Katibu wa Jumuiya hiyo Dkt. Edwin Chitage ameiambia "Father Kidevu Blog" kuwa kurejea kwa Dkt. Ulimboka akiwa mzima ni ishara ya huduma bora aliyoipata akiwa nje ya nchi.
Aidha Katibu wa Jumuiya ya madaktari Dkt. Chitage amewaahidi wanahabari kuitisha mkutano mapema ili kujuza umma wa Watanzania na dunia kwa kina kuhusu kupona Dkt. Ulimboka.
Kiongozi wa Jumuiya ya madaktari nchini Tanzania, Dkt. Steven Ulimboka, akiwa amebeba maua, na kuzungukwa na madaktari wenzake na wananchi wwengine, alipowasili nchini Jumapili Agosti 12, 2012, kwenye uwanja wa ndege wa kiamataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea kwenye matibabu Afrika Kusini. Dkt. Ulimboka alisema yuko "fit" na anaweza kufanya shughuli zozote atakazopewa kuanzia sasa. (picha: Khalfan Said)
No comments:
Post a Comment