MALAMPAKA.COM
KARIBUNI MALAMPAKA.COM
KARIBUNI
Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.
Thursday, 30 August 2012
DC aliyesema Shahada ya Mwanasheria "Ni ya Chupi" - kuburutwa kortini
.
Kufuatia habari iliyochapishwa katika Gazeti la Majira la tarehe 29-08-2012, na mwandishi, Yusuph Mussa, Korogwe, DC wa Korogwe aliyetamka maneno hayo ataburutwa kortini.
---
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Bwana Mrisho Gumbo, anatarajiwa kufikishwa kizimbani wakati wowote kwa madai ya kumdhalilisha Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bi Najum Tekka.
Bi Tekka alifikia uamuzi huo baada ya Bwana Gambo kumwambia Shahada yake ni ya nguo za ndani pamoja na kumuweka chini ya ulinzi wa polisi ili ahojiwe bila kujua kosa lake.
Akizungumza na gazeti la MAJIRA jana, Bi Tekka alisema kutokana na udhalilishaji huo, anatarajia kufungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Tanga na kudaia fidia ya Sh 90 milioni.
Alisema Juni 14 mwaka huu Bwana Gambo alimwita kwenye kikao cha kamati ya Ulinzi na Usalama cha Wilaya, ambacho kilifanyika ofisini kwake ambapo kikao hicho, pia kilihudhuriwa na baadhi ya Madiwani pamoja na viongozi wa soko la Manundu Mjini Korogwe.
Sababu ya kuitisha kikao hicho ilikuwa ni kutafuta muafaka kwa njia ya mazungumzo ili kama tutakukubaliana na wafanyabiashara wa soko la hili ambao wanapinga ongezeko la kodi ya vibanda kutoka 2,000/= kwa mwezi hadi 20,000/= kwa mwezi ifutwe.
"Majibu yangu katika kikao hiki ndiyo yalimfanya Bwana Gambo kunidhalilisha kwani mimi kama mwanasheria sina uwezo wa kuzungumza kesi ambayo ipo mahakamani," alisema Bi Tekka.
Alisema baada ya kuzungumza maneno hayo Bwana Gambo alianza kusema, "Huyu Mwanasheria Digrii yake ni ya Chupi, sina imani naye kabisa, kesi zote za halmashauri anazisababisha yeye, hana msaada wowote kwetu."
"Kimsingi amenidhalilisha mimi mwenyewe pamoja na taaluma yangu kwa maneno aliyoyatumia, pia amenidhalilisha kwa kuniweka chini ya ulinzi wa polisi ili nihojiwe wakati kosa langu mimi silijui hata mahakamani sijapelekwa" alisema Bi. Tekka.
Bi Tekka alisema pamoja na kumpa bwana Gambo siku 14 awe amefuta kauli yake kwa kuitisha kikao kama alichokiitisha awali bado alipuuza, mbali na kushauriwa na wakuu wenzake wa wilaya.
"Nafungua kesi Kesho (jana) Mahakama Kuu kanda ya Tanga, ili aweze kunilipa Milioni 90 kwa kunidhalilisha" alisema
Bwana Gambo alipofuatwa na MAJIRA alikiri kumualika Bi. Tekka kwenye kikao hicho ili aweze kutoa ufafanuzi kwanini wameshindwa kufikia muafaka na wafanyabiashara.
"Kabla ya hapo mimi niliwaita wafanyabiashara wakakubali kwenda kufuta kesi, lakini huyu mwanasheria sijui ana maslahi gani na kesi hii, tulishafikia mwafaka na waende mahakamani kuifuta lakini walipofika akawakimbia. Hadi sasa kesi haijafutwa lakini wafanyabiashara wamekubali kulipa Sh. 10,000/= badala ya Sh.20,000/=, kweli aliandika notice ya kuomba radhi kwa kumdhalilisha lakini nilimwambia aende mahakamani hata leo, tutakwenda kupambana " alisema Gambo.
Bwana Gambo alipongeza kuwa, kama Bi.Tekka anadai alidhalilishwa, mbona hakuandika madai hayo polisi badala yake anakaa na watu wake na kudai amedhalilishwa?
Prosper R Mushi
No comments:
Post a Comment
Newer Post
Older Post
Home
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment