KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday, 23 August 2012

Twite aipamba Yanga Kigali 


Beki mpya wa Yanga, Mbuyu Twite akifanya mazoezi jana asubuhi kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali. Yanga leo itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports. Picha na Doris Maliyaga.
























Doris Maliyaga, Kigali 
BEKI mpya wa Yanga, Mbuyu Twite jana asubuhi alianza mazoezi rasmi na mabingwa wa Kombe la Kagame ambao leo watashuka dimbani kuivaa Rayon Sports kwenye Uwanja wa Amaholo jijini Kigali.

Katika siku za karibuni Mbuyu alitawala vichwa vya habari vya magazeti kufuatia sakata lake la kujiunga na Yanga muda mfupi baada ya Simba kutangaza kumsajili. 

Akizungumzia na Mwananchi, Mbuyu alisema anajisikia vizuri kuungana na wachezaji wenzake na kuomba kupewa ushirikiano ili wafanikiwe kutwaa mataji mengi zaidi.

"Nimefurahi kujiunga na wenzangu, najisikia furaha kuwa nao na naahidi kushirikiana nao vizuri ili kuipa Yanga mataji ,"alisema Mbuyu aliyekuwa amevaa jezi namba 9 mgongoni wakati wa mazoezi hayo.

Naye kocha mkuu wa Yanga, Tom Saintfiet alisema,"Mbuyu ni mchezaji mzuri naamini ataisaidia Yanga, lakini hiyo yote itatokana na juhudi zake pamoja na wenzake."

Kocha Saintfiet alisema katika mchezo wao wa leo anategemea Mbuyu ataanzia benchi kwa kuwa ndio kwanza ameanza mazoezi na wenzake.

"Mazingira ya kambi ni mazuri, uwanja ni mzuri na tumefanya mazoezi kwa siku mbili (juzi na jana) na kesho (leo) tunacheza mechi bila shida," alisema Saintfiet.

Alisema,"mechi hiyo ni muhimu kwetu kwa sababu timu tunayocheza nayo ni nzuri na ina ushindani, naamini tutapata mazoezi ya kutosha hapa Kigali." 

Katika mazoezi ya jana asubuhi kwenye Uwanja wa Amaholo, Yanga walianza kwa kukimbia na kufanya mazoezi ya viungo baada ya hapo, Saintfiet aliwataka wachezaji kucheza kwa nafasi na walitumia nusu Uwanja pamoja na kupiga mashuti.

Baada ya hapo walicheza mpira kwa mtindo wa mechi katika vikosi viwili tofauti.

Kwa mujibu wa mazoezi ya jana kikosi cha Yanga kitakuwa hivi katika mechi ya leo: Ally Mustapha, Shadrack Nsajigwa, Oscar Joshua, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Nizar Khalfan.

No comments:

Post a Comment