Kaimu Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu (CWT), Ezekiah Oluoch ametangaza kujiuzulu wadhifa wake ndani ya chama hicho iwapo Serikali itathibitisha kuwa kuna shinikizo la chama chochote cha siasa katika utendaji kazi wa viongozi wa chama hicho.
Kauli hiyo ya Oluoch imekuja siku kadhaa baada ya kuibuka tuhuma kuwa migomo inayoandaliwa na CWT kushinikiza walimu kudai nyongeza ya mshahara imekuwa na msukumo kutoka kwa vingozi wa CHADEMA.
Alidai tuhuma hizo tayari amezisikia kuwa yeye na Rais wa CWT wanashinikizwa na CHADEMA kuwataka walimu kugoma wakidai nyongeza ya mishahara yao, “Niko tayari kujiuzulu wadhifa wangu iwapo vyombo vya Dola vitabaini tumekuwa tukiwasiliana na viongozi wa CHADEMA katika kuanzisha hii migomo, wachunguze namba zangu za simu, utendaji wangu wa kazi na wanifuatilie kwa namna yoyote wakinithibitishia hata kidogo basi naachia ngazi,” alisema Oluoch.
Alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani Rukwa baada ya ziara yake mikoani yenye lengo la kufanya tathmini ya mgomo wa walimu uliofanyika hivi karibuni kabla ya kuzuiwa na Mahakama Kuu kwa madai ya kukiukwa kwa kanuni na sheria kabla ya kutangazwa kwa mgomo huo.
Alisema mara kadhaa CWT inapotangaza kupambana na Serikali katika kudai haki za wanachama wake, kumekuwa kukiibuka maneno mengi huku viongozi wake wakituhumiwa kushinikizwa na viongozi wa chama fulani cha siasa jambo ambalo si la kweli, “CWT ni chama huru, hivyo kazi yake kubwa ni kuhakikisha maslahi ya wanachama yanatekelezwa lakini wanatimiza wajibu wao kwa Serikali, hivyo kutangaza mgomo ni haki yake na tulizingatia sheria ya Ajira na Mahusiano kazini ya mwaka 2004,” alisema.
Pia alisema CWT inakusudia kuwasilisha rufaa kwenye Mahakama ya Rufaa wiki ijayo, kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu inayoeleza kuwa mgomo wake uliotangazwa hivi karibuni ulikuwa batili.
Katika hukumu hiyo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam iliamuru CWT kusitisha mgomo wa walimu walioutangaza kote nchini lakini pia wakitakiwa kulipa fidia kwa hasara zote zilizotokea wakati wa mgomo huo.
Alisema rufaa ya kupinga hukumu hiyo ilikuwa iwasilishwe mapema, lakini walikuwa wakisubiri Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwasilisha hotuba ya Wizara yake bungeni ili wabunge wapate fursa ya kuchangia kwa upana, badala ya kuzuiwa kujadili kiundani.
Tulijua iwapo kesi hiyo ingekuwa imefunguliwa, Spika angewazuia wabunge kujadili kwa upana kwenye hotuba hiyo, hivyo wiki ijayo utakuwa ni wakati muafaka wa kufungua kesi ya kukata rufaa,” alisema.
via HabariLeo

No comments:
Post a Comment