Ferguson akasirika RVP kutopewa ushirikiano |
LONDON, England KOCHA wa Manchester United, Alex Ferguson amewalaumu wachezaji wake kwa kushindwa kumtumia Robin van Persie baada ya kufungwa bao 1-0 na Everton. Van Persie aliingia akitokea benchi dakika ya 68, wakati tayari United wameshafungwa bao na Marouane Fellaini kwenye Uwanja wa Goodison Park Jumatatu usiku. Mshambuliaji huyo wa Uholanzi ambaye amekamilisha usajili wake wa Pauni 24 milioni kutoka Arsenal Ijumaa iliyopita, alishindwa kuisaidia timu yake hiyo mpya isipate kipigo hicho cha kwanza tangu walipofungwa kama ilivyokuwa mwaka 2004. "Tulicheza kwa kumsogelea zaidi yeye na tukashindwa kutengeneza nafasi nzuri zaidi kwa Robin kutumia uwezo wake wa kuwatoroka mabeki, tulishindwa kumtumia vizuri zaidi," alisema Ferguson. Ferguson alifafanua sababu ya kumwazisha benchi Van Persie kwa kusisitiza kuwa mshambuliaji huyo hakupata muda mwingi wa kucheza wakati wa mazoezi ya mwanzo wa msimu. "Hakufanya maandalizi ya kutosha ya mwanzo wa msimu, ndiyo maana niliona ni bora akaanza benchi ili apate kuona namna wenzake wanavyocheza," alisema. "Ni mchezaji mzuri na kila wakati unapokuwa na mchezaji kama huyu unashawishika kuanza kumtumia haraka, lakini ni vyema kama utamweka benchi." Kipa wa United, David de Gea alifanya kazi kubwa kuokoa hatari kadhaa kutoka kwa washambuliaji wa Everton waliokuwa na uchu wa kufunga mabao mengi. Kiungo Leon Osman alikuwa nyota kwa wenyeji, lakini Ferguson alikiri kuwa wachezaji wake walishindwa kumzuia mfungaji Fellaini. "Ni mchezaji mkubwa, mrefu anayejua kutumia vizuri mipira ya juu jambo lililowapa wakati mgumu mabeki wangu," alisema. "Walimtumia vizuri wakati wote kwa kupitisha mipira kwake na mwishowe walifanikiwa kupata bao kupitia yeye." Kocha wa Everton, David Moyes aliwapongeza wachezaji wake kwa kupata ushindi huo, lakini hakuzungumzia chochote kuhusu ushindi huo wa kwanza wa Everton kuupata mwanzo wa msimu tangu mwaka 2007. Moyes alivutiwa zaidi na kiwango cha juu kilichoonyeshwa na kiungo wa Japan, Shinji Kagawa katika mchezo huo. "United wamefanya usajili mzuri msimu huu," aliongeza Moyes. "Kiungo wa Japan ameonyesha kiwango cha juu |
No comments:
Post a Comment