KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Monday, 20 August 2012


Yanga Yaicharaza African Lyon 4-0

 
Beki wa timu ya Yanga, Oscar Joshua (kulia) akimtoka mshambuliaji wa African Lyon, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo jioni. Katika mchezo huo Yanga imeibuka na ushindi wa Mabao 4-0. Bao la kwanza la Yanga, limefungwa na kipa wa African Lyon, Juma Abdul, aliyejifunga katika dakika 8, kipindi cha kwanza, bao la pili limefungwa na Haruna Niyonzima kwa mkwaju wa penati, dakika ya 54, baada ya beki wa Lyon Semi Kessy, kumchezea rafu, Msuva katika eneo la hatari. Goli la tatu limefungwa na Simon Msuva, katika dakika ya 72, kufuatia pasi safi ya Frank Dumayo na bao la nne limefungwa na Jerry Tegete katika dakika ya 90+2, baada ya pasi safi ya Idrisa Rashid.


 
Kikosi cha timu ya Africa Lyon kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mpambano huo kuanza.


 
Kikosi cha timu ya Yanga kikiwa katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa Taifa kabla ya kuingia uwanjani. Chanzo: www.fullshangweblog.com

No comments:

Post a Comment