Picha za siku ya pili ya ziara Rais Kikwete nchini Canada asaini FIPA kulinda Canadians in TZ
Rais Kikwete akipanda mti katika bustani ya Jumba la Rideau Hall jijini
Rais Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la askari shujaa katika bustani ya Confederation Square jijini Otttawa Alhamisi Octoba 4, 2012
Rais Kikwete akisimama wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa mara baada ya kuweka shada la maua katika kaburi la askari shujaa katika bustani ya Confederation Square jijini Ottawa Alhamisi Octoba 4, 2012. Mbele yake ni baadhi ya veterani wa kijeshi waliohudhuria hafla hiyo.
Rais Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kupokelewa katika Bunge la Seneti la Canada. Kulia ni Spika wa Bunge hilo Mhe Noel Kinsella, anayefuatiwa na Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper na Spika wa Bunge la wawakilishi la Canada (House of Commons), Mhe Andrew Scheer pamoja na viongozi wengine wa bunge hilo Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo, ambapo viongozi hayo wawili walifanya mazungumzo Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Kikwete na Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper
Rais Kikwete akimpa zawadi ya sanduku la Zanzibar (Zanzibar chest) Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Kikwete akioneshwa na Spika wa Bunge la Seneti la Canada ramani ya dunia na njia za meli, pamoja na kuoneshwa chemba ya mikutano ya Maseneta wa Bunge la Canada Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Kikwete akikaribishwa katika ofisi ya Spika wa Bunge la Wawakilishi la Canada (House of Commons) Mhe Andrew Sheer. Spika huyu, mwenye umri wa miaka 32, ndiye kiongozi kijana kuliko wote katika historia ya nchi hiyo waliopata kuchaguliwa kuongoza bunge hilo.
Rais Kikwete na mwenyeji wake Stephen Harper wakitembea kuelekea kwenye chumba cha mkutano kuongea na wanahabari. Zuria jekundu na bendera za Canada za kiongozi wa nchi husika huwekwa sehemu hiyo kwa heshima na wakati wa ziara ya kiongozi wa nchi ya nje aliye katika ziara rasmi nchini humo
Rais Kikwete na mwenyeji wake Stephen Harper wakishudia uwekaji sahihi mkataba wa ushirikiano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mhe. Bernard Membe na Waziri wa Canada katika Bunge la seneti la nchi hiyo Alhamisi Oktoba 4, 2012
Rais Kikwete na mwenyeji wake Stephen Harper wakiongea na wanahabari katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo
Rais Kikwete, Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa pili mbele kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe Alex Massinda (mbele kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa makampuni ya Canada baada ya mazungumzo katika jengo la Rideau Hall jijini Ottawa
Rais Kikwete akiongea na mabalozi wa nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini Canada, na baadaye kupiga nao picha ya pamoja.
Rais Kikwete akiwa na Watanzania Richard Katambi Masalu na mkewe Patricia katika jengo la Rideau Hall jijini Ottawa kabla ya kuondoka kuelekea Edmonton
Prime Minister Stephen Harper and Jakaya Kikwete, ident of Tanzania, chat in the Library of Parliament during President Kikwete's State Visit to Canada. October 4, 2012. (Photo by Jason Ransom)Prime Minister Stephen Harper and Jakaya Kikwete, President of Tanzania, chat in the Library of Parliament during President Kikwete's State Visit to Canada. October 4, 2012. (Photo by Jason Ransom)
No comments:
Post a Comment