KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday, 19 July 2012



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana huko Chumbwe wakati Rais na Mama Salma Kikwete walipowatembelea kuwafariji na kuwapa pole katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja leo Julai 19, 2012.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembelea Uwanja wa Maisara, Zanzibar, ambako ndiko miili ya marehemu huletwa kwa utambuzi baada ya kuokolewa kwenye eneo la ajali leo Julai 19, 2012.


Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimsikiliza mmoja wa walionusurika katika ajali ya meli jana Bw Kitwana Makama Haji ambaye kalazwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja leo Julai 19, 2012




Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole Bi Salome Abeli, mmoja wa walionusurika katika ajali hiyo ya meli. Yeye ni mfanyakazi wa Tanzania Automic Energy Commission akitokea Arusha kwenda Pemba Kikazi leo Julai 19, 2012.






PICHA: IKULU


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Khamis Haji Khamis, jinsi ulivyandaliwa utaratibu wa kuwahifadhi marehemu watakaokosa kutambuliwa na ndugu zao, wakati Makamu alipofika kwenye Viwanja vya Maisara mjini Zanzibar, leo Julai 19, 2012, kuangalia shughuli za uokoaji na utambuzi wa marehemu. Kushoto ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza mmoja kati ya vijana walionusulika katika ajali ya Meli ya Skagit, Kitwana Makame Ali (24) mkazi wa Unguja, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, leo Julai 19, 2012 kuwafariji wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo baada ya kuokolewa katika ajali hiyo iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe. Kulia ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano, Samia Suluhu Hassan.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza mmoja kati ya vijana walionusulika katika ajali ya Meli ya Skagit, Masembe Enos (32), mkazi wa jijini Mwanza aliyekuwa akisafiri na mkewe ambaye mpaka sasa hajapatikana.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mgonjwa aliyenusulika katika ajali ya Meli ya Skagit, Hamisa Akida (45) mkazi wa Ununio mjini Bagamoyo, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza mmoja kati ya vijana walionusulika katika ajali ya Meli ya Skagit, Stephano Lufyagila (22), mkazi wa Kiwalani jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na vijana wawili, Hans Manoni (kulia) na Nsunga Joseph, waliokuwa wakisafiri na wenzao wawili ambao wamefariki katika ajali hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsalimia Salome Abeid Mwambaga (33) mkazi wa jijini Arusha, mfanyakazi wa Kampuni ya Atomic Enegy Commissioner, aliyekuwa akisafiri kuelekea Pemba kikazi ambaye pia amepoteza vifaa vya kazi na Document zake zote muhimu katika ajali hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, wakati alipofika Ikulu mjini Zanzibar leo kwa ajili ya kumpa pole kuhusu ajali ya Meli ya Skagit mali ya Kampuni ya seagull, iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe.

Wananchi wakiwa wamepanga foleni kuelekea kutambua miili ya marehemu katika Viwanja vya Maisara leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kujionea shughuli hizo katika viwanja vya Maisara mjini Unguja leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumjuika na wananchi katika moja ya familia iliyopotelewa na ndugu katika ajali hiyo, mjini Zanzibar leo mchana.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mgonjwa aliyenusulika katika ajali ya Meli ya Skagit, Hamisa Akida (45) mkazi wa Ununio mjini Bagamoyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, wakati alipofika Ikulu mjini Zanzibar leo Julai 19, 2012 kwa ajili ya kumpa pole kuhusu ajali ya Meli ya Skiget mali ya Kampuni ya seagull, iliyotokea jana eneo la Kisiwa cha Chumbe.

[Picha na Muhidin Sufiani-OMR]


No comments:

Post a Comment