KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Wednesday, 18 July 2012


 Mbunge wa Mwibara, ambaye ni polisi mstaafu, Kangi Lugola (CCM), ametoa shutuma nzito bungeni akisema kuna mtandao mkubwa wa uhalifu unaohusisha askari Polisi huku akimtaja kwa jina, akisema ndiye kinara.

Katika hatua nyingine Mbunge huyo amesema daima Polisi itaendelea kuwa nyuma ya wahalifu na ni ndoto kukabiliana na majambazi kwa vile inatumia mbinu na zana dhaifu ikilinganishwa na teknolojia na umahiri wa mbinu za majambazi.

Alisema hayo bungeni mjini hapa jana alipochangia hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi kuhusu mapato, makadirio na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2012/13.

Huku akimtaja Fadhil Kweka, kuwa askari anayeongoza mtandao huo huku akiahidi kutoa ushahidi. Hata hivyo, hakuna mbunge aliyesimama kuomba Mwongozo wa Spika kutokana na Lugola kumtaja Kweka ambaye hana nafasi ya kujitetea.

Lugola alisema ni lazima Serikali ikomeshe mtandao huo wa askari wanaojihusisha na uhalifu mara moja vinginevyo ni ndoto kwa uhalifu kumalizika.

via HabariLeo


No comments:

Post a Comment