KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Sunday, 29 July 2012

WACHEZAJI WA YANGA NA RAHA YA UBINGWA WA KAGAME CUP LEO.
Wachezaji wa timu ya Yanga wakishangilia na kombe lao walilokabidhiwa leo mara baada ya kuifunga timu ya Azam FC katika mchezo uliokuwa ni wa kuvutia kwa timu zote baada ya kuitandika timu ya Azam magoli 2-0 kwenye mchezo wa fainali katika michuano ya kombe la Kagame iliyomalizika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
 
 
 
Wachezaji wa timu ya Azam ambayo imechukua nafasi ya pili wakipita jukwaani na kupewa medali zao baada ya mchezo huo kumalizika jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa.
 
 
 
Wachezaji wa timu ya Vita kutoka DRC Congo wakipta jukwaani na kupokea medali zao Vita wamechukua nafasi ya tau baada ya kuifunga timu ya APR ya Rwanda katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu uliofanyika kalba ya mchezo wa fainali.

No comments:

Post a Comment