Mchezaji wa timu ya Yanga Stefano Mwasika akikokota mpira kuelekea goli la timu ya Mafunzo ya Zanzibar huku beki wa timu ya Mafunzo Ismail Khamis Amour wakati timu hizo zikichuana katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Kagame unaofanyika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa, mpira umekwisha na timu ya Yanga imeshinda kwa penati 5-3 baada ya kutoka suluhu katika kipindi cha dakika tisini za mchezo huo, magoli 1-1 ambapo timu ya Mafunzo ilijipatia goli lake kupitia mchezaji Ali Othman Mpemba katika dakika ya 35 kipindi cha kwanza huku lile la Yanga likifungwa na Said Bahanuzi katika dakika ya 46 kipindi cha pili, ndipo baada ya dakika tisini penati zikapigwa Yanga kufanikiwa kuifunga Mafunzo kwa matuta
Ubao ukionyesha matokeo baada ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo.
Kikosi cha timu ya Mafunzo ya Zanzibar kikiwa katika picha ya pamoja
Kikosi cha timu ya Yanga kikiwa katika picha ya pamoja. Chanzo: www.fullshangweblog.com
No comments:
Post a Comment