na Abdallah Khamis
MBUNGE wa Kigamboni, Dk Faustine Ndungulile (CCM) amechaguliwa kuwa
mwakilishi wa Bara la Afrika kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Masuala ya Ukimwi
(IAS) ambapo atashikilia nafasi hiyo kwa muda wa miaka minne.
Hiyo ni mara
ya pili kwa Dk. Ndungulile kushika nafasi hiyo baada ya kipindi cha mwaka 2008 -
2012 kumalizika.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Dk. Ndungulile, ilieleza
alichuana na wagombea wengine 13 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambazo ni
Ethiopia, Nigeria, Afrika Kusini, Rwanda, Kenya, Morocco, Sudan na Misri.
Alisema majukumu ya taasisi hiyo yenye makao makuu yake Geneva, Uswisi ni
pamoja na kuhamasisha njia bora na ya kisasa katika mapambano dhidi ya ukimwi,
kutoa elimu na kujenga uwezo wa wataalamu wa ukimwi katika vita dhidi ya ugonjwa
huo.
No comments:
Post a Comment