KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday, 6 September 2012


JK Apewa Tuzo Ya Uongozi Bora

 

 

 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhiwa Tuzo ya Uongozi Bora wa sera ya Kilimo na Chakula toka kwa  Bw. Ajay VAshee, Makamu Mwenyekiti wa asasi isiyo ya kiserikali inayohusika na sera za  kilimo na chakula na Maliasili n ijulikanayo kama Food, Agriculture and Natural Resources Policy (FANRPAN) katika hoteli ya White Sands jana Septemba 5, 2012.  Anayeshuhudia kulia ni Katibu Mtendaji wa FANRPAN) Dkt Lindiwe Sibanda. Tuzo hiyo, ambayo hutolewa kwa kiongozi aliyefanya juhudi kuhakikisha kuwepo kwa sera bora  za kilimo na chakula nchini kwake, ilichukuliwa na Malkia Ntombi Indlovukazi wa Swaziland mwaka jana, wakati Rais Hifikepunye Pohamba alitunukiwa mwaka 2010, Rais Armando Emilio Gwebuza mwaka 2009 na  Rais wa Malawi, Hayati Bingu Wa Mutharika, aliipokea mwaka 2008.
 

  
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia baadhi ya ng'ombe anaowafuga kwa kufuata njia za kisasa kwenye shamba lake kijijini kwake Msoga, Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, leo Septemba 6, 2012.


PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment