KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Wednesday, 19 September 2012


RAIS KIKWETE AMTEUA RISHED BADE KUWA NAIBU KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA).


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Rished Bade (pichani) kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Taarifa iliyotolewa Jumatano, Septemba 19, 2012 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu, imesema kuwa uteuzi huo umeanza Jumatatu wiki hii, Septemba 17, 2012.
Kabla ya uteuzi wake, Bwana Bade alikuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TanzaniaMortgage Finance Co. Ltd.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
19 Septemba, 2012

No comments:

Post a Comment