PICHA ZA MATUKIO YA KIKAO CHA NEC YA CCM KINACHOENDELEA MJINI DODOMA
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kabla ya kikao cha NEC, leo mjini Dodoma. Wengine, waliokaa. Kutoka kushoto ni Mawaziri Wakuu wa zamani, John Malecela na Cleopa Msuya, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Sheni, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi na Kulia ni Mawaziri wakuu wa zamani Frederick Sumaye na Edward Lowassa. (Picha na Bashir Nkoromo).
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wana-CCM, alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akishiriki kucheza wimbo wa hamasa ya Chama, alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akishiriki kucheza wimbo wa hamasa ya Chama, alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifuatana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Sheni baada ya kuwasili Chama, alipowasili kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akishauriana jambo na Katibu Mkuu wa CCM, WisoMakamu (kushoto) baada ya kupiga picha ya pamoja na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, leo, kwenye viwanja vya Ofisi ya Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma. Wengine Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yussuf Makamba na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Sheni.
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akishauriana jambo na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ukumbini kabla ya kuanza kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Samwel Sitta akimsalimia kwa unyenyekevu Mjumbe mwenzake, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya, nje ya ukumbi, kabla ya kikao cha NEC mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa NEC, Frederick Sumaye akimweleza jambo Mjumbe wa NEC mwenzake Kingune Ngombale-Mwilu, baada ya kukutana nje ya ukumbi, kabla ya kikao cha NEC mjini Dodoma leo.
Baadhi ya wajumbe wa NEC wakiwa ukumbini kwenye kikao cha NEC mjini Dodoma leo.
No comments:
Post a Comment