KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Wednesday, 26 September 2012


JK Alipowaapisha Maofisa wa JWTZ 

 Amirijeshi Mkuu, Jakaya Kikwete akimwapisha Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba (kulia) kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu leo jijini Dar es salaam. Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Abdulrahaman Shimbo aliyestaafu utumishi jeshini kwa Umri.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akimwapisha Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga (kulia) kuwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) leo Ikulu jijini Dar es salaam
  Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto) na maofisa wa Jeshi Luteni Jenerali Samuel Ndomba, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ (wa tatu kutoka kushoto) na Meja Jenerali Raphael Mugoya Muhuga mkuu wa JKT walioapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Maofisa wa JWTZ na Jeshi la Kujenga Taifa leo  mara baada ya hafla fupi ya kuwaapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Samuel Ndomba na Mkuu wa JKT Meja Jenerali Raphael Muhuga.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Devis Mwamunyange (kushoto) akimweleza jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (kulia) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam.Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (katikati).
 Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel Albert Ndomba akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kuapishwa leo jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) akiwaeleza jambo viongozi wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, mkuu wa Jeshi la Polisi (wa pili kutoka kulia) na Paul Chagonja kamishina wa Oparesheni. Kulia ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Devis Mwamunyange.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Maofisa waandamizi wanawake wa JWTZ leo Ikulu jijini Dar es salaam. Kulia ni Meja Jenerali Lilian Kingazi (Kulia) na Meja Jenerali Grace Mwakipunda (kulia). Picha zote na Aron Msigwa – MAELEZO.

No comments:

Post a Comment