KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Wednesday, 12 September 2012


MATUKIO MBALIMBALI YA MKUTANO WA 14 WA MAZINGIRA UNAOZINDULIWA LEO JIJINI ARUSHA.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Anna Maembe  (wa kwanza kulia) akijianidkisha kushiriki mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Mazingira barani Afrika ambao unazinduliwa leo jijini Arusha na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Gharib Bilal.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nkoanrua ya wilayani Arumeru ambao ni wadau wa Mazingira shuleni hapo kwa kushirikiana na YVE Tanzania wakisubiri kushiriki Mkutano wa Mazingira leo jijini Arusha.
Mwakilishi wa MO BLOG Bw. Mahmoud Ahmad akizungumza na wanafunzi sekondari Nkoanrua ya wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.
Wageni watakaoshiriki mkutano wa mazingira wakiperuzi mitandao katika ukumbi wa mikutano wa AICC.
Wadau kutoka NEMC wakijadiliana jambo.
Wataalam kutoka mtandao wa mazingira ulio chini ya NEMC ambao utazinduliwa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Gharib Bilal. Pichani Kulia ni Dkt. Christopher Muhando na kushoto ni Bw. Obadia Machupa.
Wadau kutoka NEMC wakiaanda sehemu yao ya kutoa maelezo kwa wadau mbalimbali wa mazingira kutoka nchi 53 za Afrika.
Mtaalamu wa Mazingira kutoka Gabon Bi. Marie Rosine Itsana.
Pichani ni Wawakilishi kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
Vodacom nao wapo kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wageni wanaohudhuria mkutano wa 14 wa Mazingira barani Afrika unaozinduliwa rasmi leo mchana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment