MAONYESHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI YAENDELEA MKOANI IRINGA
Wananchi mbalimbali wakipata maelezo kutoka kwa ofisa wa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani katika banda la la kikosi hicho kwenye maonyesho ya wiki ya Nenda kwa usalama Barabarani yanayofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa, maadhimisho hayo yalizinduliwa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Dk Emmanuel Nchimbi.
Ispekta Agatha Isaack kushoto wa kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu Dar es salaam akizungumza na maafisa wenzake katikati ni Afande John Chacha na Afande Sajenti Valentine Ngowi kutoka makao makuu.
Banda la Kikosi cha usalama Barabarani likiwa limefurikwa wananchi na wanafunzi mbalimbali ili kujifunza mambo mbalimbali kuhusu sheria za usalama Barabarani.
No comments:
Post a Comment