WATANZANIA WATAKIWA KUTAFAKARI JUU YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal akifungua mkutano wa 14 wa Mawaziri wa Mazingira barani Afrika jijini Arusha.
Mahmoud Ahmad Arusha
Makamu wa raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Mohamed Gharib Bilal amewataka watanzania kuanza kwanza kutafakari na kuangalia suala zima la kupambana na tabaka la Mmong’onyoko wa gesi ya okaa Angani Ozon na mabadiliko ya tabianchi sanjari na utunzaji wa mazingira.
Makamu wa rais ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa 14 wa mazingira jijini Arusha huku akitanabaisha kuwa mataifa ya kiafrika yanawajibu mkubwa wa kutunza mazingira yake ya asili katika kuweka vyanzo vya mazao ili kuweka usalama wa chakula kwa watu wa mataifa hayo.
“tutaendelezaje mazingira yetu katika kuendeleza kukua kwa uchumi na uchumi wenyewe ni ule wa kijani kwa mataifa yetu ya kiafrika sanjari na utunzaji wa mazingira yetu”alisema makamu wa raisi.
Makamu wa raisi alienda mbali kwa kusema kuwa ifike mahali tukayahami mazingira yetu ilikuleta ustawi kwa jamii yetu na kuweka mkazo kuviendeleza vyombo vyote vinavyosimamia mazingira kwenye mataifa yetu hususani hapa nchini.
Dkt. Bilal alisema kuwa tuweze kujali mazingira kuanzia sehemu tunamoishi na kuangalia tabaka mbali mbali ilikuweza kufanikiwa katika kutunza mazingira na kutanabaisha kuwa nchi nyingi za kiafrika suala la uchumi limekuwa likiwafanyakushindwa kufikia malengo ya utunzaji wa mazingira.
Dkt Gharib alisema kuwa kama hatutasaidiwa kiuchumi na mashirika ya kifedha ulimwenguni nchi nyingi za kiafrika zitadorora katika suala zima la utunzaji wa mazingira na kuyaomba mataifa yaliyoendelea kuendelea kusaidia mataifa ya kiafrika iliyaweze kufikia malengo ya utunzaji wa mazingira.
No comments:
Post a Comment