MAZISHI YA BABA WA TUNDU ANTIPAS LISSU
Wakili wa kujitegemea mkoani Arusha, akisoma taarifa ya wasifu wa baba yake mzee Augustino Lissu Mughwai (86) wakati wa misa ya mazishi wa mzee huyo ambaye pia ni mzazi wa mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu.Mzee Augustino alifariki dunia septemba 16 mwaka huu.
Waziri wa nchi, sera, uratibu na bunge Mh. William Lukuvi akitoa salamu kwenye msiba wa baba yake na mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu kijijini Mahambe.
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe (wa kwanza kulia) akifuatilia misa ya mazishi ya baba mzazi wa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu MzeeAugustino Lissu Mughwai aliyefariki dunia Septemba 16 mwaka huu.
Waziri wa nchi,sera,taratibu na bunge William Lukuvi (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye msiba wa mzee Augustino Lissu Mughwai baba mzazi wa mbunge wa jimbo la Singida mashariki Tundu Lissu.Wa kwanza kushoto ni naibu waziri wa maliasili na utalii,Lazaro Nyalandu na wa pili kushoto ni mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone.Wa kwanza kulia ni mbunge wa Karatu CHADEMA,Israel Natse.
Wakili wa kujitegema mkoani Arusha, Allute Mughwai (wa kwanza kulia) akifuatilia kwa makini misa ya mazishi ya baba yake mzee Augustino Lissu Mughwai. Wa nne kutoka kulia ni mbunge wa jimbo la Singida mashariki,Tundu Lissu.
Mbunge wa jimbo la Kigoma kaskazini Kabwe Zitto (kulia) akizungumza na mkuu wa wilaya ya Ikungi Manju Msambya wakiwa kwenye mazishi ya baba wa mbunge wa jimbo la Singida mashariki,Tundu Lissu.(Picha zote na Nathaniel Limu)
No comments:
Post a Comment