Spika Makinda na waombolezaji wengine walioshiriki kwenye Msiba Wa Baba Yake Mhe. Tundu Lissu
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimfariji Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu alipofika kuhani msiba wa Marehemu baba yake Mhe. Tundu Lissu mzee Agustinio Lissu Mughwai Nyumbani kwake tegeta, Dar es Salaam. Mzee Lissu alifariki Jumapili tarehe 16 Septemba, 2012, katika Hospitali ya Muhimbili, Dar es salaam na anatarajiwa kuzikwa jumamosi Singida
Spika wa Bunge akisaini kitabu cha maombolezo
Mhe. Spika akimfariji mbunge wa Viti maalum Chadema
Mhe. Christina Lissu ambaye pia ni dada yake na Mhe. Tundu Lissu alipowatembelea kuhani msiba wa baba yao Tegeta
Mbunge wa Singida Mjini Mhe. Tundu Lissu akiteta jambo na Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda alipofika kuhani msiba wa baba yake Mhe. Lissu Mzee Agustinio Lissu Mughwai Tegeta Dar es Salaam
Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge
MALAMPAKACOM.BLOGSPOT.COM INAUNGANA NA FAMILIA YA LISSU
KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU BWANA AMETOA BWANA
AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE
No comments:
Post a Comment