Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasili katika ukumbi wa MNelum Pokuna Mahinda Rajapaksakuhudhuria ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) uliofunguliwa leo na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa. Aliye pembeni yake ni Mjumbe wa CPA Tawi la Tanzania na Mbunge wa Kigoma Mhe. Zitto Kabwe.
Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa akihutubia Maspika, Wabunge na maafisa zaidi ya 850 kutoka Mabunge ya nchi wanachama jumuiya ya madoloa wakati wa ufunguzi rasmi wa mkutano huo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akishangaa jambo wakati wakiwa katika mazungumzo na Spika wa Kenya Mhe. Kenneth Marende mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa CPA unaofanyika nchini Sri Lanka
Mhe. Zitto Kabwe akiteta jambo na Mbunge toka Uganda (hakufahamika jina mara moja) pamoja na Spika wa Bunge la Malawi Mhe. Henry Chimundu Banda (katikati) mara baada ya ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 58 wa CPA unaofanyika nchini Sri Lanka. Kulia ni Mhe. Hamad Rashid Mjumbe wa CPA tawi la Tanzania
Wajumbe wote wa Mkutano wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi leo
Spika wa Bunge. Mhe. Anne Makinda akiteta jambo na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pande Ameir Kificho pamoja na Mhe. Zitto Kabwe wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 58 wa Chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA) leo Mjini Colombo, Sri Lanka. Mkutano huo umefunguliwa rasmi na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa. Wa Kwanza kulia ni Afisa dawati wa CPA tawi la Tanzania Ndg. Said Yakubu

No comments:
Post a Comment