KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Sunday 12 August 2012

Malawi: hatutapigana 



Waandishi Wetu
MALAWI imesema imeondoa ndege zake zilizokuwa zikifanya utafiti wa mafuta katika Ziwa Nyasa kwa kuwa haitaki kuingia vitani, badala yake imeamua kupeleka mgogoro huo Mahakama ya Kimataifa.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Mambo ya Ndani na Uhusiano wa Kimataifa kwa Mambo ya Kiusalama wa Malawi, Uladi Mussa alipokuwa akizungumza na gazeti linalochapishwa nchini humo la Nyasa Times.
“Nawahakikishia wananchi mtaendelea kuishi kwa utulivu. Tupo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania, bila shaka mambo yataenda vizuri. Kama hali ikishindikana tutalipeleka suala hili kwenye Mahakama ya Haki ya Kimataifa,” alisema Mussa.
Kauli ya Waziri huyo imekuja wakati baadhi ya wananchi wa Malawi wanaoishi katika Vijiji vya Karonga na Chitipa vilivyopo kando ya Ziwa Nyasa upande wa Malawi wakiwa wameanza kuvihama vijiji hivyo kuhofia usalama wa maisha yao.

Baadhi ya wakazi hao wamekaririwa na Nyasa Times wakisema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo kunusuru maisha kutokana na kuwapo kwa dalili za kutokea vita kati ya Malawi na Tanzania.
Waziri Mussa amesema suala hilo la mgogoro wa mpaka litaamuliwa kwa njia ya amani na hivyo kuwataka wananchi kuendelea na shughuli zao bila wasiwasi.


Waziri huyo aliwahakikishia wananchi hao kuwa Serikali ya Malawi ina ushahidi wa kutosha kuwa ziwa lote la Malawi (Nyasa)ni mali ya Malawi na Tanzania haina nguvu ya kuwasimamisha kuendelea na kazi ya kutafuta mafuta.
“Kimsingi hapa hakuna hoja ya kubishania. Wote tunajua ziwa hili ni mali yetu (Malawi),” alisema. 
“Kama malalamiko haya yangekuwa yametolewa na Msumbiji, hapa tungekuwa na hoja ya kubishania, lakini si Tanzania.” alisisitiza.

Alisema ushahidi wao wa mipaka ni wa tangu mwaka 1890 wakati ambako wakoloni wa Uingereza na Ujerumani walitiliana saini juu ya suala hilo.
Aliendelea kueleza kuwa umiliki huo wa ziwa  umeongezewa nguvu na maazimio ya mwaka 1963 ya Wakuu wa uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika (OAU) kwamba wanachama wanapaswa kuheshimu mipaka waliyorithi kwa wakoloni.

Kauli za wananchi
Wakati Serikali ya Malawi ikitoa msimamo huo watu kadhaa waliohojiwa wameonyesha hofu ya nchi hizo kuingia katika vita.

Heckley Christopher ambaye ni raia wa Malawi anayefanya biashara eneo la Mbambabay mkoani Ruvuma anasema: " Malawi ni nchi ndogo sana kupigana na Tanzania, ni nchi yenye mikoa minne tu, kukiwa na vita itaangamia mara moja."
Raia mwingine wa Malawi ni Vilion Gordon ambaye alisema Tanzania na Malawi ni marafiki wa siku nyingi, hivyo hawana sababu za kugombania ziwa ambalo lilikuwapo tangu enzi hizo.

"Nashauri wakae chini wapatane, kwa nini tugombane sasa wakati ziwa hilo lilikuwapo tangu enzi hizo?"alisema.
Mtanzania mkazi wa Kijiji Lundo kilichoko Mbambabay mkoani Ruvuma, Zakhia Chengula ameitaka Serikali ya Tanzania kuendelea kuimarisha ulinzi na kukubali kuingia katika mazungumzo na Malawi badala ya kufikiri vita.
"Hapa sisi ni kwetu, vita ikiingia sisi tutakufa tu hakuna pa kukimbilia. Tunaiomba Serikali iimarishe ulinzi eneo hilo na ikae na Malawi kuzungumzia mgogoro huo," alisema.

Mkuu wa Wilaya mpya ya Nyasa, Ernest Kahindi alisema hakuna hofu yoyote kwa wakazi wanaoishi kando ya Ziwa Nyasa upande wa Tanzania.
Amewataka wananchi hao kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali kama kawaida kwani suala hilo sasa linashughukiliwa kitaifa.

"Mwanzoni kulikuwa na hofu kubwa, lakini baada ya Serikali ya Tanzania kutoa tamko la kutaka ndege za Malawi ziondoke na zenyewe kutii amri hiyo, hakuna tatizo lolote," alisema na kuendelea;
"Shughuli katika eneo hili zinaendelea kama kawaida. hakuna mwananchi aliyepigwa risasi wala ndege iliyotunguliwa, mambo yako shwari."
Jeshi laimarisha ulinzi

Katika hatua nyingine Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limeimarisha ulinzi katika mwambao wa Ziwa Nyasa na kupiga marufuku wananchi kukatisha eneo lao la jeshi.

Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Kyela waliozungumza na gazeti hili jana walisema kuibuka kwa mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi, kumesababisha kuongezeka kwa ulinzi katika eneo hilo.

“Mara ya kwanza tulikuwa tunaingia tu pale kambini kama tumeagizwa vitu kama mayai, vocha na vitu vingine na wanajeshi wa pale  tunawapelekea, lakini sasa tangu kuibuka kwa mgogoro huo wa mpaka wa Ziwa Nyasa na hawa wa Malawi tumezuiliwa kabisa kuingia hapa” alisema mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa jina Hamis

Chanzo cha hofu

Jumatatu wiki hii, akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe aliitaka Malawi kuziondoa ndege na kampuni zinazofanya utafiti wa mafuta katika eneo hilo kwa kuwa ni mali ya Tanzania.

“Serikali ya Tanzania inapenda kuyaonya na kuyataka makampuni yote yanayoendelea na shughuli za utafiti eneo hilo zisitishe mara moja kuanzia leo (Jumatatu),” alisisitiza Membe.

Mbali na Waziri Membe viongozi wengine waliozungumzia mgogoro huo na kuitaka Malawi iache uchokozi ni Samuel Sitta na Mwenyeti wa Kamati ya Bunge ya masuala ya ulinzi, Edward Lowassa.

Wakati Sitta akiwataka Watanzania kuendelea nashughuli zao bila hofu kwa kuwa Serikali iko tayari kwa tishio lolote, Lowassa alisisitiza kuwaTanzania imejiandaa kiakili na kivifaa kuingia vitani na Malawi kama italazimika kufanya hivyo.
Habari hii imetayarishwa na Joyce Joliga, Nyasa, Godfrey Kahango, Kyela, Leon Bahati na Mashirika ya Habari


 

Comments 

 
0#22 burton 2012-08-12 10:10
Hu ni mgonganisho kutoka kwa wazungu ili tupigane wapate kuza silaa,pia uyo rais wao kawekwa kwa shnkzo la waingereza ndiomana akaruhusu ndoa za jinsia moja kwaiyo anataka ku2fanya nasi kama wao,hakuna kukubali serikali kwa njia yoyote ile haki itendeke,
Quote
 
 
0#21 Ushindi 2012-08-12 03:43
Hawa wazungu ndio wanotuharibia kila kitu.Mikataba yao haikujali haku za binadamu,waliga wana mipaka yetu kwa maslahi yao.Sizani kama Malawi na Tanzania waliwahi kugombania Ziwa hili kabla hawajaja hawa makabaila.
Sasa naona watakuwa nyuma ya Malawi,na hiyo kampuni inayofanya uchunguzi watakuwa na vithibitisho vya mipaka kutoka uingereza ili kuhakikisha wanafyonza mafuta yoooooote hadi ya upande Tanzania.
Hapa hakuna haja ya kugombana. ni 50% kwa 50%
Quote
 
 
0#20 scout boy tz 2012-08-12 02:46
Ndugu zangu watanzania wapendwa,huyu kiongozi wa malawi hatutakii mema tangulini wewe uka miliki water body ambayo imeigusa nchinyingine kwamfano yakitokea mafuriko wamalawi watakuja ku kuzuia maji watanzania waishio kando ya ziwa wasi asirike inawezekana? pia ukweli ni kwamba hauwezi kuzuia maji maana hatakama huo mpaka utaupitishaje maana maji kutokana na utafiti huwa yana kula kingo zake kwahiyo baada ya miaka 50 ijayo mpaka utakuwa umefika mbeya mjini lol! mimi nashauri kama wakiendelea wasimamishwe kwa nguvu zote.go jwtz go....
Quote
 
 
0#19 jj 2012-08-12 01:23
lowasa mwanaumeeeeeeee eeeee
Quote
 
 
0#18 jxmaduhu 2012-08-12 01:20
they did intentionally,h uku wakijua ni kosa.kauri ya jk nyerere itumike wasipoelewa.sababu ya kuwapiga tunayo,nia ya kuwapiga na uwezo wa kuwapiga tunao,hivyo wapewe siku za kukanusha kauri yao vinginevyo wapigwa
Quote
 
 
0#17 Mwalimu Chauled 2012-08-11 20:44
Inawezekana kabisa Rais wa malawi na waziri wake hawajui kusoma ramani. Ziwa nyasa lipo katikati ya Tz na malawi. Itafikia hatua hata Burundi na DRC watadai ziwa Tanganyika la kwao. Kama wataweza mziki wa Bongo wajaribu waone, waulize uganda kilichowapata! Sembuse kamalawi kanalingana na mkoa wa kilimanjaro au Morogoro.
Quote
 
 
0#16 Mkumba 2012-08-11 19:31
Wamalawi ni ndugu zetu na ni marafiki ,kumbuka hilo viongozi wetu msije kulisahau hata mara moja. Vita ikianza mmalawi atakufa na mtanzania pia atakufa,busara itumike
Quote
 
 
0#15 miraji uliza 2012-08-11 19:04
kwa heshima ya tanzania duniani naiomba malawi isituvuvunjie heshima yetu na kama itasubutu basi kuipiga na kuisambalatisha malawi yote kuwa tanzania.
Quote
 
 
0#14 msakila kabende 2012-08-11 18:54
Tutapoteza kila ki2 na cyo ardhi na ziwa! mama umekwisha na unakuja kusahaulika kabisa
Quote
 
 
0#13 msakila kabende 2012-08-11 18:52
Hawaijui TANZANIA, kabla ya mwaka mpya tutakuwa tunakula chakula cha mchana Bulawayo na Lilongwe

Hapa kama ilivyokuwa kwa uganda tunaweka rekodi ya kuitawala malawi kwa miezi kadhaa kabla hatujawachaguli a rais baada ya kumwondoa mama huyo laghai.
Quote
 
 
0#12 Msemakweli 2012-08-11 16:11
apigwe huyu mmalawi, ameona watanzania ni wapole sasa anatishia nyau, anatingisha kiberiti aone kama tutaongea au laaa... NIA TUNAYO, NGUVU TUNAYO NA SABABU YA KUMPIGA TUNAYO!!! Huyu MWANAMAMA, AENDE AKAMUULIZE DADAA NDULI IDD AMINI...KILIMPATA, WAMALAWI WAKICHEZA, HAKA KA-NCHI KAO KATAKUWA KOLONI LA WATANGANYIKA!!!
Quote
 
 
0#11 Maiwana Hassan 2012-08-11 14:38
kwa nini Malawi asiadabishwe?... JK toa ruhusa tusafishe njia sisi.
Quote
 
 
-1#10 optatus kasogela 2012-08-10 15:48
mimi kama mtanzania mzalendo wa nchi yangu napaza sauti kwa serikali yetu nikisema...."mwondoshe...mwondoshe....msulubishe"!
Quote
 
 
+1#9 Albaert 2012-08-10 12:45
Mlawi ni wakorofi, Hata ramani inasoma hivyo toka zamani iweje leo waseme ziwa lao baada ya kuona kuna mafuta na gesi? waache tamaa.
Quote
 
 
+1#8 sadickwarsaw 2012-08-10 11:55
natumai busara zitatumika na mwafaka utapatikana kwa amani
Quote
 

Add comment

No comments:

Post a Comment