KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday 30 August 2012


BENKI YA CRDB YAFUNGUA TAWI JIPYA TABATA

 
 Tawi jipya la Benki ya CRDB Tabata jijini Dar es Salaam
 
 
Meneja wa tawi la CRDB Tabata, Hawa Sasya akiwa Ofisini 
Meneja wa Biashara za Kibenki, Burtony Mbogella 
 
 Ofisa wa Benki ya CRDB tawi la Tabata, Angel Kissanga akimuhudumia mteja
 
 Meneja wa tawi la CRDB Tabata (wa tatu kushoto) akitoa maelekezo ya huduma  mbalimbali za kibenki kwa baadhi ya wateja waliofika katika tawi hilo
 
 
 Baadhi ya wateja wakipata huduma katika tawi la benki ya CRDB Tabata
 
 
 
Ofisa wa Benki ya CRDB tawi la Tabata, Angel Kissanga akiwa kazini 
  

Na Mwandishi Wetu 
BENKI ya CRDB, imeamua kuwafikia Wakazi wa Tabata kwa kufungua tawi jipya eneo la Tabata Megengeni jijini Dar es Salaam ambapo takribani wateja 300 hupata huduma kutoka katika tawi hilo kwa siku. 
  Tawi hilo limeshaanza kufanyakazi tangu Julai 2 mwaka huu, ambapo limeonekana kuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa Tabata na maeneo ya jirani. 
 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa tawi hilo, Hawa Sasya amesema kuwa wateja wa Tabata na maeneo ya jirani sasa wanaweza kupata huduma za kibenki katika tawi hilo. 
 Alifafanua kwamba, tangu kuanzishwa kwake tawi limekuwa ni mkombozi kwa wateja mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo na Makanisa, Misikiti na watu mbalimbali. 
  “Tawi lipo karibu na Kanisa la Kristo Mfalme, Tabata Magengeni, ambapo linatoa huduma mbalimbali zikiwemo za; Mashine ya kutoa na kuweka fedha (ATM) ambayo hufanyakazi kwa muda wa saa 24”alisema 
  Alitaja huduma zingine kuwa ni pamoja na TemboCardVisa, Akaunti ya Hundi na ya watoto inayojulikana kama Junior Account pamoja na Akaunti ya Akiba. 
  Hata hivyo aliongeza kuwa, tawi hilo litakuwa likitoa Akaunti ya Tanzanite, na huduma za mikopo mbalimbali na huduma za bima. 
  Alisema kuwa tangu kuanzishwa kwake tawi limekuwa likitoa huduma ya kibenki kwa kutumia Simu ya mkononi (SimBanking), pamoja na Akaunti ya Wanafunzi ambayo inafahamika kama Scholar Account. 
  Meneja huyo aliwataka Wananchi na wateja wapya kutumia tawi hilo pekee katika eneo la Tabata ili kupata huduma za kibenki badala ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo kwenye matawi yaliyombali.

No comments:

Post a Comment