KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Sunday 26 August 2012


 
Picture
MKURUGENZI Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Bw. Eric Shigongo, anasikitika kutangaza kifo cha baba yake mzazi na Mwenyekiti wa Global Publishers Ltd, Mzee James Bukumbi, kilichotokea usiku wa kuamkia Jumapili Tarehe 26/8/2012 katika Hospitali ya Burhani jijini Dar es Salaam.

Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwake Kijitonyama, Barabara ya Sayansi, jirani na Heko Motel, Dar es salaam.
Marehemu atasafirishwa kwenda Mwanza kwa mazishi Jumanne 28/8/2012 na maziko yatafanyika kijijini kwake Bupandwamhela, Sengerema, Mwanza.

Habari ziwafikie ndugu wote wa ukoo wa Bukumbi popote walipo, ndugu wa ukoo wote wa Kapera popote walipo, wananchi wote wa Jimbo la Buchosa, ndugu, jamaa na marafiki wa Shigongo popote walipo


No comments:

Post a Comment