MKUU MKOA WA SINGIDA DR. KONE ATEMBELEA WIZARA YA FEDHA KATIKA MAONYESHO YA WAKULIMA YA NANENANE MJINI DODOMA
Mkuu wa Mkoa wa
Singida,Dr. Parseko Kone (kushoto) akitaka kujua maoni kutoka kwa Mhasibu wa
Wizara ya Fedha Abbas Myeto(kulia)kuhusu taratibu za kupata pesheni kwa
watumishi wa umma wanapostaafu . Mkuu huyo wa Nkoa wa Singida aliomba ufafanuzi
huyo leo alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima
kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa
Singida, DK. Parseko Kone (kushoto) akitaka kujua jana mjini Dodoma kutoka kwa
watendaji wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) kwanini kuna utofauti
wa ubora katika bendera ya Taifa ya kuweka katika magari kwa viongozi. Mkuu Mkoa
huyo aliuliza swali hilo leo alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika
maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma. Aliyeshika
bendera ndogo ya taifa ni Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Mikataba Maalum
Modecai Mato (kulia).
Mkuu wa Mkoa wa
Singida, Dk Parseko Kone (kushoto) akipata maelezo mafupi jinsi Wakala wa
Huduma ya Ununuzi Serikalini [GPSA] inavyosaidia katika kudhibiti matumizi
mabaya ya fedha za umma yaliyokuwa yakifanyika kupitia ununuzi wa vifaa
mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya ofisi za serikali na taasisi zake. Mkuu Mkoa
huyo alipata maelezo hayo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Mikataba
Maalum Modecai Mato (kulia) jana alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika
maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma.
Mchambuzi wa
Mifumo ya Komputya Mkuu Daraja la III kutoka Idara ya Menejimenti ya TEKNOHAMA
ya kifedha , Wizara ya Fedha Margethi Ambrosi Nembo (kushoto) akitoa maelezo kwa
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr. Parseko Kone (kulia) leo mjini Dodoma jinsi
kuingiza mishahara na malimbikizo ya watumishi wa umma kwa kutumia TEKNOHAMA .
Mkuu Mkoa huyo alikuwa katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.




No comments:
Post a Comment