Naibu katibu mkuu wa UVCCM Zanzibar, Jamal Kasim Ally
(kulia) akimkabithi fomu za kugombea nafasi ya uongozi wa UVCCM-NEC Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Bw Jerry Silaa jana katika ofisi za CCM mkoa mjini
Magharibi Zanzibar, katikati ni Bw Abdallah Mwinyi-katibu wa vijana mkoa Kusini
unguja akishuhudia tukio hilo. UVCCM -NEC imetangaza nafasi zinazogomewa kua ni
Mwenyekiti, Mkamu mwenyekiti, Katibu, Wajumbe wa Baraza Kuu na wajumbe wa
Halmashauri. Hata hivo mstahiki meya wa manispaa ya ilala alipohojiwa hakuweka
wazi nafasi gani anayotaka kugombea kwani alikua bado anakusanya maoni na
ushauri kutoka watanzania mbalimbali na kujipima mwenyewe ni nafasi ipi itakayo
mfaa zaidi ili kuweza kuwatumikia wananchi vema.Tetesi kutoka kwa wadau wake wa
karibu zinasema mstahiki meya anataka kugombea nafasi ya Mwenyekiti
UVCCM-NEC.
No comments:
Post a Comment