WABUNGE WAGAWANYIKA NA KUZUSHA MJADALA MKALI JUU YA FAO LA KUJITOA.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe akichangia kwa hisia katika semina ya wabunge juu ya fao la kujitoa, kwenye ofisi za bunge mjini Dodoma leo.
Na. Mwandishi wetu-Dodoma.
Wabunge wa bunge la Tanzania wamegawanyika katika semina yao juu ya fao la kujitoa katika mifuko ya hifadhi ya jamii ambapo wabunge wengi vijana wanataka mifuko hiyo irudishe sheria ya kujitoa wakati mawaziri na baadhi ya wabunge wengine wanakataa kurudishwa kwa fao hilo.
Kuna hoja zingine za wabunge zinazotaka sheria ya fao la kujitoa lisiwepo na badala yake kuwepo fao lingine la kujikimu kwa wanachama wanaoachishwa kazi wakati wakisubiri umri wao wa kupata fao la kujitioa.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zito Kabwe (Chadema) amesema kuwa kwa sasa fedha nyingi za mifuko ya hifadhi ya jamii zinatumika vibaya kwa kisingizio cha uwekezaji na masuala mengine yanayofanana na hayo na kusababisha hofu kubwa ya uwezo wa mifuko hiyo kuwalipa wanachama wake hapo baadaye.
Amesema kuwa yeye hatakuwa tayari kuona kuwa mifuko hiyo haina fedha ya kuwalipa wanachama wanaofikisha umri wa kupata fao la kujitoa, endapo kama atakuwa Rais wa nchi yetu ya Tanzania .
Zito amesema kuwa hata kama siye yeye atakuwa Rais wa Tanzania miaka ijayo, laikini hatapenda kuona mtu yeyote atakayekuwa Rais akishindwa kuwalipa mafao wanachama wa mifuko hiyo.
Usemi wa Zitto ulileta minong’ono kutoka kwa wabunge na Spika aliyekuwa anahudhuria semina hiyo katika ukumbi wa zamani wa Bunge kwa sasa unaitwa ukumbi wa Pius Msekwa.
No comments:
Post a Comment