Bodi Ya Utalii Washuhudia Matangazo Yao Uingereza
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Uingereza na Mbunge wa Jimbo la South Shields, Mh. David Miliband wakati ujumbe wa TTB ulipotembelea Uwanja wa Sunderland FC na kushuhudia mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza kati ya timu hiyo na timu ya Aston Villa uliofanyika siku ya Jumamosi nchini Uingereza. Bodi ya Utalii Tanzania inatangaza matangazo ya utalii wa Tanzania katika viwanja sita vinavyotumika kuchezea Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League) ukiwemo Stadium of Light wa Sunderland FC. Katika picha katikati ni Edmund Hazal, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lantech Services inayoratibu matangazo hayo. Bw. David Miliband pia ni Mwenyekti wa Klabu ya Sunderland.
Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Uingereza na Mbunge wa Jimbo la South Shields, Mh. David Miliband akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB, Bw. Geofrey Meena (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza kati ya Suderland na Aston Villa. David Miliband pia ni mwenyekiti wa klabu ya Suderland.
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devotha Mdachi, akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani na maofisa wa timu ya Sunderland FC baada ya kukabidhiwa zawadi ya saa. Kutoka kulia ni Balozi wa Sunderland na golikipa wa zamani Jimmy Montgomery, Gary Mutchinson, Mkurugenzi wa Biashara, na Kevin Ball nahodha wa zamani wa timu hiyo.
Ujumbe wa Bodi ya Utalii na maofisa wa taasisi mbalimbali wakipiga picha ya pamoja nje ya uwanja huo. Kutoka kulia ni Manase kutoka Ngorongoro, Mukhtar kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Masoko TTB Devotha Mdachi, Geofrey Meena Meneja Masoko TTB na Edmund Hazal, Mkurugenzi wa kampuni ya Lantech Services inayoratibu matangazo hayo katika viwanja vya Ligi Kuu Uingereza.
Picha kwa hisani ya Fullshangweblog
No comments:
Post a Comment