KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Tuesday, 27 November 2012


Hospitali 37 Kunufaika Na Bilioni Kutoka Uholanzi

 
 Balozi wa Uholanzi nchini Dr. Ad Koekkoek (kulia) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam kuhusu msaada wa shilingi bilioni 33 uliotolewa na Uholanzi kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili kuimarisha huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali katika Hospitali 37 hapa nchini . Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah. Tanzania nayo inatakiwa kuchangia kiasi kama hicho katika huduma hiyo ili kuwa asilimia 50 kwa 50 kila pande yaani Tanzania na uholanzi.
 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam kuhusu msaada wa shilingi bilioni 33 uliotolewa na Uholanzi kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili kuimarisha huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali katika Hospitali 37 hapa nchini. Kulia ni Balozi wa Uholanzi nchini Dr. Ad Koekkoek . Tanzania nayo inatakiwa kuchangia kiasi kama hicho katika huduma hiyo ili kuwa asilimia 50 kwa 50 kila pande yaani Tanzania na Uholanzi.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah (kushoto) na Balozi wa Uholanzi nchini Dr. Ad Koekkoek (kulia) wakibadilishana hati ya msaada wa shilingi bilioni 33 uliotolewa na Serikali ya Uholanzi kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili kuimarisha huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali katika Hospitali 37 hapa nchini. Tanzania nayo inatakiwa kuchangia kiasi kama hicho katika huduma hiyo ili kuwa asilimia 50 kwa 50 kila pande yaani Tanzania na Uholanzi.
         Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salaam


TANZANIA imepokea msaada wa shilingi bilioni 33 kwa ajili kusaidia uboreshaji wa huduma za uchunguzi wa afya kwa kipindi cha miaka mitano ijayo hapa nchini.
 
Msaada huo huo utawezesha Serikali ya Tanzania kuboresha huduma ya uchunguzi katika hospitali 37 kwa ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kufanyia uchunguzi ambavyo vitawasaidia wataalam kutoka matokeo matatizo yanayowakabili wagonjwa kwa haraka zaidi .
 
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dar es salaam mara baada ya kupokea msaada huo kutoka Ubalozi wa Uholanzi hapa nchini kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Ramadhan Khijjah alisema kuwa Tanzania alisema kuwa msaada huo utaiwezesha Serikali kunulia vifaa vya kufanyia uchunguzi wa kisasa kama vile kununulia vifaa vya X-ray na ultrasound ambazo vitasambazwa katika Hospitali hizo
 
Alisema kuwa msaada huo ni muhimu kwa Serikali ya Tanzania kwani utaisaidia Serikali kupunguza gharama ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa wale wanaohitaji kupatiwa huduma za uchunguzi wa kina wa afya zao badala yake kazi itafanyika hapa nchini mara baada ya ununuzi wa vifaa hivyo.
Khijah alisema katika makubaliano Serikali ya Tanzania nayo itachangia kiasi hicho fedha katika msaada huo ili kufanikisha ununuzi wa vifaa vya huduma ya uchunguzi .
 
Alisema kuwa msaada huo utadumu kwa kipindi cha miaka mitano ambapo mara baada ya miaka hiyo kumalizika Serikali ya Tanzania itausimia yenyewe .
 
Alitaja mikoa itakayonufaika na msaada huo ni pamoja na Shinyanga, Kagera, Iringa, Mwanza, Pwani, Lindi, Mtwara, Dar es Salaam, Arusha, Dodoma, Kigoma, Manyara, Mbeya, Morogoro, Kilimanjaro, Mara, Rukwa, Singida, Ruvuma, Tanga na Tabora. Kufuatia hali hiyo Katibu Mkuu huyo aliwataka watendaji wa Hospitali zote zitakazonufaika na msaada huo kuwa makini katika utunzaji wa vifaa ili viweze kutumika kwa muda mrefu na uboreshaji wa afya za wananchi.
 
Naye Balozi wa Uholanzi nchini Dkt. Ad Koekkoek alisema kuwa msaada huo unalenga upatikanaji wa huduma za bora za ultra sound, CT scan ,na x-ray hapa nchini na hivyo kuboresha huduma za afya.
Aliongeza kuwa huduma hiyo inalenga kuufanya uchunguzi wa magonjwa uwe wa kisasa zaidi ambapo wataalam wataweza kufanya uchunguzi kwa haraka na kama kama utahijika sehemu nyingine kuweza kuutuma kwa njia mtandao(internet).

No comments:

Post a Comment