Dkt.Bilal Afungua Mkutano Wa Bima
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa Blue Peal, jijini Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kufungua mkutano wa 8 wa Kimataifa wa Bima, ulioanza leo Novemba 6, 2012 ukitarajia kumalizika Novemba 8, mwaka huu.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wa Kimataiafa wa Bima, kutoka mataifa mbalimbali wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia, katika ukumbi wa Blue Peal, leo Novemba 6, 2012
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua mkutano wa 8 wa Kimataifa wa Bima, ulioanza leo Novemba 6, 2012 katika ukumbi wa Blue Peal, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo unatarajia kumalizika Novemba 8 mwaka huu. Picha na OMR
No comments:
Post a Comment