HATMA YA OBAMA NA ROMNEY KUJULIKANA BAADA YA UCHAGUZI WA RAIS LEO.
Barack Obama na Mitt Romney.
Wananchi wa Marekani leo wanapiga kura kuchagua rais mpya, huku wagombea Mitt Romney wa Republican na rais Barack Obama wakichuana katika kinyang’anyiro kikali katika miongo kadhaa.
Kura za maoni zinaonyesha Obama amesogea mbele ya mpinzani wake kwa asilimia ndogo lakini uchaguzi huu wa Jumanne utaamuliwa wakati wa mwisho.
Chama cha Republican kimelalamikia tufani ya Sandy iliyoikumba Marekani wiki iliyopita, ambayo wanasema ilipunguza kasi ya kampeni ya Romney.
Wagombea wote wanafanya ngwe za mwisho mwisho katika majimbo yenye maamuzi, wakitarajia kuwashawishi wapiga kura ambao hawajaamua nani wa kumchagua.
No comments:
Post a Comment