KIIZA: SINA MPANGO WA KUHAMIA SIMBA.
Striker wa Yanga Hamis Kiiza amekanusha uvumi ulioenezwa na magezeti ya hapa nyumbani ya kuwa anahamia timu ya mabingwa wa tetezi wa ligi kuu bara Simba katika dirisha dogo la usajiri lililofunguliwa siku ya jumatano.
Fununu zinazoenea zinada Kiiza yupo katika mazungumzo na Simba wakati huohuo Azam FC wameonesha nia ya kumuhitaji. Lakini hivi ndivyo asemavyo mwenyewe
“sinampango wa kwenda popote, mimi bado ni mchezaji wa Yanga kisheria na yeyote mwenye kuhitaji sahihi yangu ni lazima awaone mabosi wangu Yanga.. Bado nina mkataba nao na ninauheshimu sana.
Kiiza ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Uganda tayari ameifungia Yanga magoli matatu katika msimu huu na anatarajia kururi Uganda mwisho wa wiki hii kwaajili ya Cecafa Senior Challenge Cup, mashindano yatakayofanyika mwisho wa mwezi huu.
No comments:
Post a Comment