BALOZI PETER KALLAGHE AKUTANA NA MAAFISA WA BODI YA UTALII TTB NA UBALOZI KUJADILI MAANDALIZI YA USHIRIKI WA TANZANIA MAONYESHO YA (WTM) JIJINI LONDON
Mh.Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Balozi Peter Kallaghe leo ameitisha mkutano kati yake na maafisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na maafisa wa Ubalozi ili kuzungumza nao na kupata taarifa muhimu juu ya maadandalizi ya ushiriki wa Tanzania katika maonyesho ya utalii ya (WTM), yanayotarajiwa kuanza siku ya jumatatu Novema 5 mpaka Novemba 8 mwaka huu katika jiji la London.
Maonyesho ya Utalii ya (WTM) yanayoandaliwa nchini Uingereza ni maonyesho makubwa na yanashirikisha makampuni kutoka mataifa mbalimbali duniani kwa ajili ya kuuza bidhaa zao, hasa Mahoteli, Makampuni ya Ndege na makampuni ya Utalii, Mwaka huu Tanzania inashirikisha makampuni zaidi ya 55 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
Katika picha juu akisisitiza jambo katika mkutano huo, wakati wa mkutano huo ambapo aliza kila jambo ambalo linahitaji kupata majwabu muhimu kabla ya kuanza kwa maonyesho hayo.
Maafisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza wakimsikiliza kwa makini Mh. Balozi Peter Kallaghe wakati akiongea nao katika mkutano huo
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena akifafanua jambo katika mkutano huo, kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Devotha Mdachi.
Bi Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) akimfafanulia jambo Mh. Balozi Peter Kallaghe wakati wa mkutano huo katika ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza.
No comments:
Post a Comment