KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday, 15 November 2012


BODI YA UTALII TANZANIA (TTB) YAZINDUA MKAKATI WA KUTANGAZA UTALII KIMATAIFA


Waziri wa maliasili na Utali Mh. Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika uzinduzi  wa Mkakati wa mpya wa Utangazaji wa Kimataifa wa Utalii wa Tanzania (International Marketing Strategy For Tanzania)mpango uliozinduliwa jioni hii na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam na kujumuisha wadau mbalimbali wanaojihusisha na masuala ya utalii ambapo Waziri Kagasheki ameuzindua rasmi.
(PICHA NAWWW.FULLSHANGWEBLOG,COM)
Waziri wa maliasili na Utali Mh. Balozi Khamis Kagasheki akikata utepe katika kitabu kinachoelezea mkakati wa kutangaza utalii wa utalii wa Tanzania kimataifa kutoka kulia ni Bw. Gaudence Temu Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania (TCT), Ahmad Khatib Kamishna wa Utalii na kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dkt. Aloyce Nzuki.
Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Balozi Charles Sanga akizungumza katika uzinduzi huo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dkt. Aloyce Nzuki  akimkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii ili kuzungumza na wageni waalikwa na wadau mbalimbali katika uzinduzi huo.
Bw. Gaudence Temu Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Utalii Tanzania (TCT) akielezea mkakati wa kutangaza utalii wa Tanzania kimataifa kwa wadau wa masuala ya utalii waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Ibrahim Mussa  akikaribishwa katika uzinduzi huo na Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi. Devotha Mdachi
Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bw Geofrey Meena kushoto na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Utalii Tanzania (TCT) Bw. Richard Rugimbana wakifuatilia kwa karibu maelezo yaliyokuwa yakitolewa katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dkt. Aloyce Nzuki akisalimiana na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya (TTB) . Bi. Teddy Mapunda, katikati ni Godfrey Simbeye Mkurugenzi Asasi ya Sekta Binafsi Tanzania Private Sector Foundation na Dan Kisirye kutoka International Finance Corporation.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamis Kagasheki akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya utalii (TTB)Balozi Charles Sanga katikati na Mjumbe wa Bodi hiyo Bi. Teddy Mapunda.
Balozi Khamis Kagasheki akisalimiana na Mbunge wa Mafia na Mjumbe wa Bodi ya (TTB) Mh. Abdulkarim Shah
Waalikwa mbalimbali wakiwa katika hafla ya uzinduzi huo.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Utalii Tanzania (TCT) Bw. Richard Rugimbana kulia akijadiliana jambo na Dan Kisirye kutoka International Finance Corporation, katikati ni Godfrey Simbeye Mkurugenzi Asasi ya Sekta Binafsi Tanzania Private Sector Foundation.
Kutoka kulia ni wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)Karaze, Beatrice na Fatma wakiwa katika picha ya pamoja.
Mwenyekiti wa bodi ya utalii Balozi Charles Sanga akizungumza jambo na Mbunge wa Mafia na Mjumbe wa Bodi ya (TTB) Mh. Abdulkarim Shah, kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dkt Aloyce Nzuki.
Kundi la Wanne Star likitumbuiza katika uzinduzi huo
Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya utalii Tanzania (TTB) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya maofisa wa bodi ya utalii Tanzania wakiwa katika hafla hiyo wakibadilishana mawazo hapa na pale kulia ni Bw. Mussa Kopwe Mkuu wa Utawala, Bw. Deo Mkuu wa Utafiti kushoto na Bw. Kaduma Mwanasheria wa (TTB) katikati.

No comments:

Post a Comment