MAWAZIRI WA UTALII JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAZINDUA JARIDA LA KWENYE NDEGE KATIKA MAONYESHO YA (WTM) JIJINI LONDON
Waziri wa Utalii wa Kenya Mh. Danson Mwazo katikati ambaye pia ni mwenyekiti wa mawaziri wa utalii katika nchi za Afrika Mashariki na Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania Balozi Khamis Kagasheki kulia, wakionyesha jarida la Round About East Africa la kwenye ndege. linaloelezea mambo mbalimbali ya utalii na pia kutangaza utalii wa nchi za Afrika Mashariki, mara baada ya kulizindua rasmi katika hafla iliyofanyika kwenye maonyesho ya dunia ya Utalii World Travel Market (WTM) Excel Jijini London nchini Uingereza, kulia ni Waziri wa Utalii wa Utalii wa Uganda pamoja na wawakilishi wa mawaziri wa utalii wa Rwanda na Burundi
Mawaziri hao wa Utalii ktika nchi za Afrika Mashariki wakisaini jarida hilo kuashiria uzinduzi rasmi jijini London.
Waziri wa Utalii Kenya Mh. Danson Mwazo akizunguza katika hafla hiyo, katikati ni Mh. Jesca Eriyo Naibu Katibu Mkuu wa jumuiya Afrika ya Mashariki na Balozi Khamis Kagasheki Waziri wa Maliasili nchini Tanzania.
Mawaziri hao pamoja na wawakilishi kutoka Burundi na Rwanda wakionyesha jarida hilo mara baada ya uzinduzi rasmi.
No comments:
Post a Comment