Wakati akifunga kikao cha Bunge cha jioni ya leo, Spika wa Bunge hilo Bi. Anne Makinda alitangaza kuwa Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Abdallah Juma Abdallah Saddallah alipata ajali katika eneo la Tumbi, Kibaha mkoani Pwani.
Alisema kuwa ndani ya gari hilo alikuwemo Dereva wake, Naibu Waziri, Watoto pamoja na Msaidizi wa shughulil za nyumbani.
Spika ametaarifu kuwa majeruhi waliwahishwa kwenye hospitali ya Tumbi, Kibaha kwa matibabu zaidi.
No comments:
Post a Comment