Bahanunzi, Chuji ndani Stars
KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars, Kim Poulsen, jana alitangaza kikosi cha nyota 21 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya ugenini itakayochezwa Agosti 15.
Poulsen raia wa Denmark aliyepokea jahazi hilo kutoka kwa Jan Poulsen, alisema jana kuwa uteuzi wake umezingatia uwezo wa mchezaji katika mechi za hivi karibuni zikiwemo za michuano ya Kombe la Kgame.
Michuano hiyo iliyoanza Julai 14 hadi 28, Tanzania iliwakilishwa na timu nne ambazo ni Yanga, Simba, Azam na Mafunzo.
Alisema sifa za msingi kwa mchezaji anayefaa kuichezea timu hiyo, ni kufanya kwake vizuri katika klabu yake, kujituma uwanjani na nidhamu ya ndani na nje ya uwanja.
Alisema kikosi hicho kitaripoti kambini ifikapo Agosti 9, kwenye Hoteli ya Tansoma, iliyopo jijini Dar es Salaam, Agosti 8, kuanzia saa 1:00 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza siku inayofuata.
Kwa upande mwingine, Poulsen ameendelea kuwachunia nahodha wa zamani wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa ‘Fuso’ na beki tegemeo wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro.’
Wakati hao wakiendelea kuachwa, wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya DR Congo , wameitwa.
Makipa: Deogratias Munishi (Azam), nahodha Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ali (Azam).
Mabeki: Nahodha msaidizi Aggrey Morris , Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo: Athuman Idd ‘Chuji’, Frank Domayo (Yanga), Haruna Moshi, Mwinyi Kazimoto na Ramadhan Singano (Simba), Ramadhan Chombo ‘Redondo’, Mrisho Ngassa na Salum Abubakar ‘Sure boy’ (Azam) pamoja na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji: John Bocco (Azam), Said Bahanunzi, Simon Msuva (Yanga), Samata na Ulimwengu wote kutoka TP Mazembe ya DR Congo.
No comments:
Post a Comment