WABUNGE WA AFRIKA WAZIBEBESHA SERIKALI JUKUMU LA MAKAZI BORA
Spika wa Tanzania Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo leo mjini Napoli Italia wakati wa kikao cha kujadili jinsi ya kuwashirikisha wabunge katika kuboresha miji na makazi katka nchi zinazoendelea hususan bara la Afrika.
Mhe.Susan Lyimo wa Tanzania (kushoto) akizitaka serikali kuelekeza bajeti zake katika kukabiliana na uharibifu wa miji na makazi unaosababishwa na wimbi la wananchi wengi kuhamia mijini wakati miji hiyo haijaweka miundombini madhubuti. Kulia ni Mhe. James Lembeli.
Mhe. Mariam Nalubega ni mbunge kutoka Uganda, ambaye amewataka wadau wote – serikali na secta binafsi- kulishughulikia janga la makazi mabovu kwa nguvu zao zote kwa ajili ya kizazi kijacho. Ni jukumu la serikali kuwapatia wananchi wake makazi bora.
Kutoka Bunge la Afrika Mashariki ni Mhe. Nancy Absai aliyesema kwamba makazi bora na miji bora ni chanzo kizuri cha mapato kwa taifa. Serikali zisijivue jukumu la makazi bora kwa watu wake.
Wajumbe wa kikao hicho katika picha ya pamoja.
Na Prosper Minja-Bunge (kwa picha zaidi tembelea: www.prince-minja.blogspot.com
Na Prosper Minja-Bunge (kwa picha zaidi tembelea: www.prince-minja.blogspot.com
No comments:
Post a Comment