KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Sunday, 2 September 2012


MKUU WA MKOA WA SINGIDA AMLIPUA MBUNGE ANAYEPINGA KUANZISHWA VYAMA VYA MSINGI VYA USHIRIKA.


Mkuu wa wilaya ya Mkalama Edward Ole Nalenga akizungumza muda mfupi kabla hajamkaribisha mkuu wa mkoa wa Singida Dkt.Parseko Kone kuzungumza na wanachama wa Talanta SACCOS na wananchi wa Iguguno kabla ya kukabidhi matrekta makubwa 11.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi matrekta makubwa 11 kwa wanachama wa Talanta SACCOS. Matrekta hayo yametolewa mkopo na Benki ya rasilimali (TIB), mkopo ambao una thamani ya zaidi ya shilingi milioni 156.
Mkuu wa mkoa wa Singid Dkt. Parseko Kone akijaribisha kuwasha moja ya matrekta 11 yaliyotolewa mkopo kwa wanaSACCOS wa Talanta ya tarafa ya Kinyangiri.
Mwenyekiti wa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri Mayasa Salum akijaribisha kuwasha trekta lake alilokopeshwa na benki ya rasilimali (TIB).
Jumla ya matrekta 11 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 156 yaliyotolewa mkopo kwa wanachama wa Talanta SACCOS ya tarafa ya Kinyangiri wilaya ya Mkalama. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone amemlipua mbunge mmoja wa mkoa wa Singida kwa wananchi, kwa kitendo chake cha kupinga hadharani uanzishwaji  vyama vya msingi vya ushirika.
Dkt. Kone amesema baada ya yeye kutoa amri ya kupiga marufuku wafanyabiashara binafsi kununua alizeti moja kwa moja kutoka kwa wakulima, kulitokea makundi ya wafanyabiashara na baadhi ya viongozi na hasa wakuchaguliwa na wananchi kupinga amri hiyo.
Amesema zilitumika nguvu nyingi sana zilizolenga aidha yeye kama Mkuu wa mkoa au viongozi wenginewa ngazi za juu, waifute haraka iwezekanavyo amri hiyo halali.
Dkt. Kone alipoombwa kumtaja mbunge huyo, alisema atawanong’oneza siku nyingine, lakini akasema kuwa mbunge huyo amepiga kelele sana kwamba Singida hakuna vyama vya ushirika na vyombo vya habari vimekuwa vinamtangaza sana.
Amesema kutokana na kutangazwa sana huko na vyombo vya habari,imani yake ni kwamba anafahamika kwa watu wengi kuwa kipaombele chake ni wananchi waendelee kunyonywa na walaguzi.
Akifafanua zaidi, amesema mbunge huyo amekuwa kishupalia kuwa vyama vya msingi vya wakulima havipo na vilivyopo, havina mtaji.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Kone amemlipua mbunge huyo mbele ya hafla ya kukabidhi matrekta 11 kwa wanachama wa SACCOS ya Talanta ya tarafa ya Kinyangiri wilaya mpya ya Mkalama.

No comments:

Post a Comment