KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Sunday 30 September 2012


SIMBA YAICHAPA PRISON YA MBEYA 2-1 UWANJA WA TAIFA


Mchezaji wa timu ya Simba Mwinyi Kazimoto kushoto akiwania mpira mbelea ya Fred Chudu mchezaji wa timu ya Prison ya Mbeya huku refarii wa mchezo huo Paul Soleji wa Mwanza akiangalia katika mchezo wa ligi kuu unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,Hivi sasa pira umekwisha  Simba imeifunga timu ya Prison magoli 2-1, magoli ya Simba yamefungwa na wachezaji Felix Sunzu goli la kwanza na Mrisho Ngasa aliyefunga goli la pili katika kipindi cha pili , hata hivyo Simba imepata pigo lingine baada ya mchezaji wake mwingine wa kutumainiwa Amir Maftaha kupewa kadi nyekundu na mwamuzi Paul Soleji dakika chache kabla ya kumalizika kwa kipindi cha pili.
Mrisho Ngasa wa Simba kushoto na Laurian Mpalile wa Prison wakiwani mpira katika mchezo wa ligi kuu unaofanyika kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam jioni hii.
Mashabiki wa timu ya Simba  wakishangilia wakati mchezo huo unaendelea kwenye uwanja wa Taifa.
Mashabiki wa timu ya Prison  wakishangilia wakati mchezo huo unaendelea kwenye uwanja wa Taifa.

No comments:

Post a Comment