KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Wednesday 19 September 2012


SERIKALI ZANZIBAR YAKANUSHA KUTOKEA MAUAJI WAKATI WA UCHAGUZI MDOGO BUBUBU.


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema hakuna mtu aliyefariki kutokana na vurugu siku ya  Uchaguzi mdogo wa Jimbo la  Bububu uliofanyika  Jumapili iliyopita kama ililivyodaiwa. na gazeti moja   linalotolewa kila wiki  hapa nchini.
Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Afisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar na kutiwa saini na waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mheshimiwa Mohamed Aboud Mohamed (pichani)  imeeleza hadi sasa hakuna taarifa yoyote  ya kifo kilicho sababbishwa na vurugu hilo  iliyoripotiwa.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa jeshi la Polisi lilipokea taarifa ya kujeruhiwa  watu kutokana na vurugu za baadhi ya vitkundi vya wananchi  vilivyojipanga  kuwazuia wananchi wengine  kwa makusudi  kushiriki katika zoezi la kupiga kura.
Kuhusu tuhuma zilizo tolewa dhidi ya Makamo wa Pili wa Rais  katika zoezi la upigaji kura taarifa hiyo ilieleza kuwa  maelezo hayo siyo ya kweli na kwamba  zinalenga kumchafulia jina Kiongozi huyo wa ngazi za juu
Kufuatia tuhuma hizo Serikali imemtaka Mharir wa Gazeti la FAHAMU kuthibitisha kwa maandishi tuhuma walizoandika  dhidi ya Mheshimiwa Makamo wa Pili wa  Rais au kumuomba radhi kwa maandishi kupitia Gazeti lake la FAHAMU katika kipindi  kisichozidi siku saba(7) kuanzia tarehe ya taarifa hii. Vyenginevyo Serikali itachukuwa hatua zinazofaa dhidi ya wahisika wote.
Aidha taarifa hiyo imeeleza kusikitishwa kwake na taarifa zilizotolewa na  kiongozi mmoja wa Ngazi za juu wa CUF kupitia gazeti hilo kwa kumtaja  Makamo wa Pili wa Rais  kuwa kiongozi wa juu wa serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar aliyejitosa kuharibu matokeo  ya kura  kwa kuingia katika  baadhi ya vituo kama kiongozi wa Wawananchi.
Tuhuma hizo si za kweli na zisingepaswa  kutolewa na Kiongozi  wa juu  wa chama cha siasa  kwani kiongozi huyo anaelewa fika kwamba tuhuma hizo zinachafua jina la kiongozi huyo na kuhatarisha  Umoja wa Taifa Letu.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 19/09/2012.

No comments:

Post a Comment