KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Tuesday 18 September 2012


MAONYESHO YA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI YAENDELEA MKOANI IRINGA


Wananchi mbalimbali wakipata maelezo kutoka kwa ofisa wa jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani katika banda la la kikosi hicho kwenye maonyesho ya wiki ya  Nenda kwa usalama Barabarani yanayofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa, maadhimisho hayo yalizinduliwa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Dk Emmanuel Nchimbi.
Wananchi mbalimbali wapiata maelezo katika bada la Wizara ya Ujenzi.
Ispekta Agatha Isaack kushoto wa kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu Dar es salaam  akizungumza na maafisa wenzake katikati ni Afande John Chacha na Afande Sajenti Valentine Ngowi kutoka makao makuu.
Banda la Kikosi cha usalama Barabarani likiwa limefurikwa wananchi na wanafunzi mbalimbali ili kujifunza mambo mbalimbali kuhusu sheria za usalama Barabarani.
Banda la Shirika la Bima la Taifa kulia ni  Elisante Madeko Meneja Masoko na Utafiti Shirika la Bima, kulia ni Ali Mohamed Meneja wa Bima mkoa wa Iringa na mmoja wa wananchi aliyetembelea katika banda hilo  ili kupata maelezo kadhaa kuhusu huduma za shirika hilo.
Hawa ni Farasikatika banda la ASAS Diary Farm katika maonyesho hayo.
Watoto wakishangaa Ngamia katika banda la ASAS Diary Farm.
Hawa ni Nyati Maji nao wapo katika banda la ASAS DiaryWananchi mbalimbali wakiwa katika banda la ASAS Diary Farm ambapo banda hilo lina mifugo mbalimbai kwa ajili ya maonyesho ya wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayofanyika kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.

No comments:

Post a Comment