KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Monday 16 July 2012


Morogoro Mabingwa Wa Copa Coca-Cola 2012

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joe Bendera (kulia) akitabasamu huku akiinua juu kombe la ubingwa wa 2012 Copa Coca-Cola kwa msaada wa nahodha wa timu ya Morogoro Hassan Mganga wakati wa sherehe za kufunga michuano hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Timu ya Morogoro iliibuka bingwa baada kuichapa Mwanza 1-0. Wengine ni Meneja Mkazi Coca-Cola Tanzania Dimenji Olaniyan (kushoto) na Rais wa TFF Leodgar Tenga (nyuma).Menaja Mkazi Coca-Cola Tanzania Dimenji Olaniyan (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Tshs750,000/- mfungaji bora wa michuano ya Copa Coca-Cola Mtalemwa Abogasti wakati wa sherehe za ufangaji wa michuano ya Copa Coca-Copa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki

Afisa wa maendeleo ya soka katika ukanda wa Africa Mashariki na Kusini wa FIFA Ashford Mamelodi, akiwatuku waamuzi wa michuano ya Copa Coca-Cola 2012 iliyomalizika Jumapili, Julai 15 kwa Morogoro kuibuka bingwa baada ya kuifunga Mwanza 1-0.


Meneja Mkazi wa Coca-Cola Tanzania Dimenji Olaniyan akiwakabidhi medali wachezaji wa timu ya Mwanza baada ya kuibuka mshindi wa pili kwenye michuano ya Copa Coca-Cola 2012.

No comments:

Post a Comment