KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Friday 13 July 2012


DK. SLAA AJISALIMISHA POLISI

 Dk Slaa akiwa na Godbless Lema wakiingia Makao Makuu ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya Mahojiano leo. Picha na Habari Mseto Blog.

 Wakiingia katika chumba cha mahojiano.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa nje ya jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi wakimsubiri Dk. Slaa kutoka kuhojiwa.
 Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kutoka  kuhojiwa na Jeshi la Polisi. 
 Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa akitoka katika mahojiano yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

DAR ES SALAAM, Tanzania
Majira ya saa 4:27 asubuhi gari lenye namba za usajili T 875 AKS aina ya Toyota Landcruise, liliwasili katika maegesho ya wizara ya mambo ya ndani na kisha akashuka Godbles Lema,Dk Willibrod Slaa pamoja na wakili wao Dk Rugemereza Nshala, kwa pamoja wakawa wanaelekea mlango wa kuingilia ndani ya jengo hilo.
Kabla ya kuingia ndani waandishi walitaka kujua sababu za Dk Slaa pamoja na Lema kufika makao makuu ya jeshi la polisi ambapo walisema walienda kuitikia wito.
“Tumepata wito na tumeitikia tambueni mjumbe hauawi sasa ni wito wa namna gani ngoja tukawasikilize lakini na ninyi waandishi wa habari hampitwi na kitu kila sehemu mpo”alisema Dk Slaa huku akicheka.
Baada ya kufika mapokezi Dk Slaa na Lema walielekezwa kwenda chumba namba 703 ambapo walikaa kwa muda wa dakika tano na kisha wakatoka kuelekea chumba namba 808 huku ofisa wa Polisi aliyevaa kiraia akiwataka waandishi wa habari wasiwafuate.
Katika Chumba namba 808 walichoingia ofisa huyo wa Polisi aliwakaribisha huku akisikia kuwaambia Dk Slaa,Lema paomja na wakili wao Dk Nshala kuwa wakaribie ingawa eneo hilo lipo, katika ukarabati na kisha kufunga mlango.
Akiongea na waandishi wa habari msemaji wa jeshi la polisi Advera Senso, alisema Dk Slaa na wenzake wwaliitwa kwa ajili ya maelezo ya awali ya kusaidia uchunguzi dhidi ya malalamiko yao ya kuuawa.
Alisema jeshi la polisi limefungua jalada la uchunguzi na kwamba mlalamikaji ni ni lazima atoe maelezo yatakayoweza kufanyika kwa uchunguzi huo kabala ya jalada kupelekwa kwa Mwendesha mashtaka.
“Tumewaita kwa hati maalum, dhidi ya malalamiko yao naamini tutashirikiana nao kubaini ukweli na kisha tutafanyia kazi kwa kuwa wajibu wetu ni kumlinda kila mmoja hata kama atakuwa ametolea malalamiko yake chumbani”alisema Senso.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka Dk Slaa alisema suala aliloitiwa ni juu ya malalamiko yao ya kutishiwa kudhuriwa.
Alisema alichowaeleza ni kwamba wanapaswa kuyatolea kwanza maelezo ya taarifa za nyuma za kutishiwa kwao ikiwamo suala zima la kuwekewa vinasa sauti wakati akiwa mbunge mjini Dodoma.
Kila kitu kipo wazi nimewaambia kwa sasa sina maelezo mengine zaidi ya yale niliyotoa katika mkutano na waandishi wa habari, na kubwa nikawataka wanipe mrejesho wa taarifa mbali mbali za kutishiwa kwetu tulizowafikishia kabla”alisema Dk Slaa.
Wakili aliyefuatana na viongozi hao Dk. Rugemereza Nshala, alisema wateja wake wameahidi kupeleka maelezo waliyotoa mbele ya waandishi wa habari na kwamba suala la kuhojiwa ni la kisheria hivyo wananchi wasubiri kujua kitu gani kitaendelea.
Jumatatu tutaleta yale yaliyoongelewa mbele ya waandishi wa habari na wao wafanyie kazi kuanzia hapo kuhusu kuhojiwa kwa wateja wangu hapa wamekuja kuitikia wito halali hivyo tusubiri nini kitafuata”alisema Dk Nshala.
Jumapili ya wiki iliyopita Dk Slaa akiwa na viongozi wengine wakuu wa Chadema,walisema wamebaini mkakati wa makusudi wa kuwadhuru viongozi wakuu wa chama hicho, mpango waliosema unaratibiwa na baadhi ya vigogo katika idara ya usalama wa Taifa. 

No comments:

Post a Comment